Image result for kakakuona

Kwanza kakakuona Ndiye mnyama pekee duniani ambaye mwili wake wote umefunikwa na
magamba makubwa Magamba yanayofunika mwili wa mnyama huyo ni makubwa kuliko ya viumbe wengine na magamba hayo kitaalamu yameundwa na kitu ninachoitwa ‘keratin’, ambayo yanafanana na yale yanayounda kucha za binadamu na Asilimia 20 ya uzito wa mwili wa mnyama huyo unatokana na magamba.

Kakakuona hutumia magamba hayo kama silaha ya kujilinda dhidi ya maadui.
Maana ya jina hilo la kakakuona  ilianzia nchini Malaysia, Indonesia na Brunei likimaanisha kitu kinachojikunja.

Kakakuona hupenda kujikunja kama mpira. Hiyo ikiwa kama mbinu anayotumia kujilinda dhidi ya maadui. Licha ya kuwa hutumia mbinu hiyo kujilinda, lakini anapojikunja ndiyo inakuwa rahisi kwa watu kumkamata na kumbeba.

Huishi juu ya miti na katika mashimo
Baadhi ya kakakuona huishi juu ya miti, wengine hujichimbia ardhini na kuishi ndani ya mashimo.
Wengi wanaoishi juu ya miti ni wale wenye mikia mirefu wanaopatikana barani Afrika. Wengine huchimba mashimo marefu ardhini na kuishi humo ili wasikutane na binadamu.

Si rahisi kushambuliwa na wanyama wengine
Ukiachilia mbali adui yao mkubwa ambaye ni binadamu, adui wengine wa wanyama huyo ni jamii ya chui na simba.

Hata hivyo, maadui hao hushindwa kuwashambulia kakakuona kutokana na namna wanavyojilinda kwa kujikunja na jinsi mwili wao ulivyo na magamba.

Kutokana na hali, hiyo inakuwa vigumu kwa simba au wanyama wengine kuwashambulia kwa kuwala. Hakuna anayefahamu idadi ya miaka anayoishi Inakadiriwa kuwa mnyama huyo huishi kwa kipindi cha miaka 20 akiwa katika pori. Lakini hiyo ilikuwa inafahamika zamani kipindi ambacho mnyama huyo alikuwa anaonekana tofauti na sasa.

Hata hivyo, kutokana na aina ya maisha ya wanayoishi, inasemekana kuwa wanaweza wasiishi miaka mingi, licha ya kuwa bado haifahamiki kwa sasa, inawezekana wakaishi kwa miaka 20. Hutema sumu kali mithili ya tindikali Kakakuona akiona adui hujilinda kwa kujikunja, lakini akiona hali inakuwa mbaya zaidi, hutema sumu kali mithili ya tindikali inayoweza kumdhuru adui.

Pia, wakati mwingine hunyoosha mkia wake na kuuzungisha na kumkata adui aliyekaribu yake.
katika miaka 10 iliyopita Inakadiriwa kuwa kakakuona 100,000 hukamatwa kila mwaka barani Afrika na Ulaya na kuuzwa.

China na Vietnam ndizo nchi maarufu ambazo nyama na magamba yake huuzwa. Kutokana na hilo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Hifadhi za Asili (IUCN) limemweka kakakuona kwenye orodha ya wanyama walioko kwenye hatari ya kutoweka duniani.

Hawaoni vizuri Ni aina moja katika ya nane za kakakuona wenye uwezo wa kuona vizuri hasa muda wa mchana. Hawa ni wale wanaopatikana barani Afrika.

Wengine hawana uwezo wa kuona vizuri kutokana na kuwa na macho madogo.

Lakini Wana uwezo mkubwa wa kunusa na kusikia Licha ya wengine kuwa na macho madogo na kushindwa kuona vizuri, kakakuona ni mnyama mwenye uwezo mkubwa wa kusikia sauti yoyote kwa haraka kwa sababu masikio yake yameinuka. Pia, ana uwezo mkubwa wa kunusa harufu yoyote.

Ni vigumu kujamiiana
Tofauti ilivyo kwa baadhi ya wanyamaa, upande wa kakakuona tendo kujamiiana ni gumu kutokana na tofauti za kimwili kati ya jike na dume. Mwili wa kakakuona dume una uzito mkubwa zaidi ya asilimia 50 ukilinganishwa na jike. Mbali na hivyo, hawana msimu maalumu kukutana na kujamiiana, tofauti na ilivyo kwa wanyama wengine.

Uhusiano na wanyama wengine
Imezoeleka kuwa, mnyama huyo huwa karibu na wanyama wengine wa jamii yao, kwa maana ya wale wanaokula wadudu.


Hata hivyo, hivi karibuni wanasayansi wamebainisha kuwa wamekuwa karibu na wanyama kutoka jamii nyingine kama wale wanaokula nyama. 
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
 
Top