Tuanze na Vipimo
Siagi
- Kikombe 1
Unga
- Vikombe 2
Maziwa
- 1/2 (nusu) Kikombe
Mayai
- 4
Baking
Powder - 1 Kijiko cha supu
Arki
rose - kidogo
Namna Ya Kutayarisha Na
Kupika
1. Washa oveni 350 - 400 Deg C
liache lishike moto huku ukitayarisha mchanganyiko wa keki.
2. Changanya sukari na siagi
mpaka ichanganyike.
3. Mimina mayai na maziwa
uchanganye vizuri.
4. Mimina Baking Powder kwenye
unga na uchanganye vitu vyote pamoja na arki rose.
5. Endelea kuchanganya vizuri
mpaka uhakikishe vimechanganyika vizuri (unaweza kufanya bila ya mashine)
6. Chukua trey ambayo haitojaa
ukiimimina, ipake siagi na umimine mchanganyiko wako. Treya isiwe nzito sana au
nyepesi sana bali iwe wastani.
7. Ipike (Bake ) mpaka iwive.
8. Epua iache ipoe ndio ukate
kate vipande.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog
na youtube@edone tv