Image result for maajabu ya konokono
KWANZA  Konokono ni mdudu asiye na mfupa hata mmoja mwilini mwake na kazi kubwa ya jumba lake ni kumsaidia mwendo na kuulinda mwili wake na mawaa.

PILI  Konokono wanamiliki JINSI MBILI zote mbili ya kike na ya kiume na wao wanapotaka kupandana HUVIZIANA USIKU .

TATU  Nchini Japan wataaalamu wamegundua kuwa uteute anaotoa mdudu huyu ni tiba nzuri kwa ngozi ya binadamu, na sasa tiba hiyo imeanza kupendwa barani Ulaya ikitumika sana kwenye saluni kwa ajili ya kusinga (massage).

NA matokeo ya tiba hiyo inayogharimu kiasi cha dola 50 takribani (Sh 100,000.) huonekana papohapo na kwamba wadudu hao hutoa kamasi zenye protin muhimu kwa ngozi ya binadamu. 

Konokono hutambaa uso mzima na ukiongeza hela hadi mgongo wote UNATAMBALIWA na hii inaakisi hadi misuli mingine ya mwili na kukufanya ujisikie murua na mwanana kabisa.

Image result for maajabu ya konokono NNE  Wakati huku Tanzania, konokono akionekana mdudu anaetia kinyaa kwa baadhi ya watu,nchini za China na Japan wanyama hawa wamekuwa wakitumika kama kitoweo na wengi wao hufugwa na binadamu. 

(Nimewala sana Abuja kule wanatembezwa kwenye mabeseni wakipikwa huwezi kuwatambua mara moja kama ni konokono na ni watamu saaaana na supu yake ni kama supu ya pweza kwa umaarufu huku kwetu.

TANO  Watafiti Wafaransa wamebaini kwamba unga wa konkono ni tiba muhimu sana kwa vidonda vya tumbo na mg 10 tu huweza kupunguza zaidi ya 42% ya vidonda vya tumbo na pia hutibu magonjwa sugu ya kurithi ikiwemo pumu na hata kutengenezea manukato.

SITA  Nchini Papua New Guinea, Konokono kwa miongo kadhaa wametumika kama sarafu ya nchi hiyo wakati wa UJIMA lakini.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top