Related image
NA. MARTHA MAGAWA

Siku zote katika Mapenzi hatukatazi kusaidiana ila kuna wengine
wanazidisha vizinga kiasi kwamba inakuwa sio uhusiano tena ni ‘chanzo
cha Mapato’ kwa kuliona hilo mtembezi mahaba imekuandalia njia za
kufata pindi unapoona tabia hiyo imekomaa kwa mpenzi wako.


MFUNDISHE KUKUSAIDIA
Wanaume wengi wanalisahau jambo hili la kutokuwafundisha wapenzi wao wajibu wa kutoa! Utakuta kila kitu ananunua yeye, hata nauli ya
daladala analipa, wakati mpenzi wake ana kazi yake. Ifike wakati kwa
makusudi, mwanaume ampe majukumu ya kufanya mpenzi wake, hiyo
itamsaidia mwanamke kujua namna pesa zinavyokuwa hazitoshi na akaweza kubana matumizi.

KUWA BAHILI
Wapo wanaume tangu wanatongoza wanakuwa ni wafujaji wakubwa wa pesa kwa kutoa ofa na zawadi kibao. Hii inaweza kumjengea imani mpenzi wako kuwa wewe unazo! Wakati akiwa anaamini hivyo, ukweli ulionao moyoni ni kwamba huna fedha za kutosha.


Unachotakiwa kufanya mapema ni kudhibiti matumizi yako hata kama pesa zinakuwepo. Ifahamike kuwa kutoa hakusababishi uhitaji, kadiri
unavyotoa ndivyo unavyoongeza mahitaji. Weka maisha yako katikati
usijidai tajiri kumbe ni kapuku tu.

Image result for pesa katika mapenzi
MUWEKE WAZI
Mueleze wazi kuwa huna wakati mpenzi wako anakuomba na kamwe usijaribu kutoa ahadi ambazo huenda ukashindwa kuzitimiza. Usiwe mtu wa kutoa ahadi za uongo, mara nitakununulia hiki na kile. Mwanaume hatakiwi afahamike siku ana pesa au hana. Maana kuna wenzangu ambao siku za mishahara wanabadilisha hadi kutembea! Mwanamke akijua hilo naye ataongeza mizinga ili afaidi.

Elewa tu mapenzi si kukomoana, mapenzi ni kusaidiana. Jenga tabia ya
kumsaidia mwenzako ili siku moja na wewe ukiwa na tatizo akusaidie.
Kitu unachotakiwa kukiepuka ni kuwa tegemezi hadi unakuwa kero.
Kumbuka kumpiga ‘mizinga’ mpenzi wako kila mara kunapunguza mapenzi

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top