Related image
NA. MARTHA MAGAWA

Kufanya mapenzi wakati wa hedhi ni kitendo cha kujihusisha na mapenzi na msichana au mwanamke aliye katika siku zake za kisichana.

Kuna madhara mengi yanaweza yakatokea na kwa kawaida si madhuri kwa afya ya wote wawili, Hivyo kwa ushauri huwa tunapenda watu wajari sana afya zao na si kuzidumaza na kuendekeza hisia kwani hiloo ndilo kosa kubwa la vijana wengi wa siku hizi.

Sasa hapa edonetz imekuainishia baadhi ya madhara yanayoweza kutokea endapo wawili hawa wakafanya ngono wakati KE yupo katika siku zake.

 MADHARA KWA MWANAUME.
1.Kupata maambukizi katika njia ya mkojo hadi kwenye kibofu.

 2.Maambukizi katika tezi dume(Prostetits) hii inaweza kuathiri mfumo
wa uzazi wa mwanaume.

 3.Kuziba kwa njia ya mkojo.

 4.Utasa au ugumba.

 5.Ulegevu wa misuli ya uume na upungufu wa nguvu za kiume.

 6. Athari mbaya ya kisaikolojia kwa kuwa anafanya tendo katika
mazingira machafu hali itakayompelekea kutolifurahia tendo kutokana na hali ya umaji maji,utelezi, au harufu kali na mbaya na hivyo kuona
kuwa mwanamke ni mchafu.


MADHARA KWA MWANAMKE.
1. Kupatwa na mambukizi viungo vya ndani vya uzazi kama vile shingo ya kizazi,mirija ya uzazi kwa ujumla wake anaweza kuwa na tatizo la PID (PELVIC INFLAMATORY DISEASES) tatizo ambalo linaweza kuathiri mfumo wake wa uzazi.

 2. Maumivu makali ya tumbo hasa kwa wale wanaopatwa na maumivu wakati wa hedhi.

 3. Utokaji wa damu unaweza ukaongeza kuliko vile inavyotoka kwa kawaida yake.

 4. Utasa au Ugumba.

 5. Kuvimba kwa kuta za ndani za uke kwa kuwa wakati wa hedhi zenyewe huwa tayari zimevimba au kutanunuka hali pia itamsababishia maumivu kwenye uke wakati wa tendo la ndoa.

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top