Image result for wakati sahihi kwa mtoto kuota meno
Mtoto wako atakapofikisha miezi sita, ataanza kuota meno. Watoto wengine huanza  kuudhika kwani huumia kabla meno hayajatokea kwa ufizi. Watoto wengi humwaga mate sana na hutaka kutafunatafuna vitu. Wakati mwingine watoto hutapika au kuhara wakiota meno.

Kwa kawaida kuota meno hakufanyi mtoto kupandwa na joto. Kama mtoto wako atapata joto. Kama mtoto wako atapata joto, yaweza kuwa jambo lingine. Hakikisha umemwona daktari wa watoto.
Image result for wakati sahihi kwa mtoto kuota meno
Mawaidha wakati mtoto anaota meno
  • Wakati wa kulala, weka kitambaa safi chini ya kichwa cha mwanao ambapo ule utamwagika. Unaweza kibadilisha kitambaa hichi kitakapo loweka ute.

  • Mpatie mtoto kitu cha kutafuna ambacho hakitamdhuru. Usimpatie kitu kidogo sana kwani anaweza kukimeza. Unaweza kumpatia vidunde vya mpira visivyokuwa na majimaji ndani kwani vyaweza kupasuka. Unaweza kumpa kijiko cha mpira au kitambaa safi.

  • Usifungilie kidunde cha kutafuna kwa shingo ya mwanao. Kinaweza kushikwa na kummyonga.

  • Kuna dawa nyingi dukani za kupiunguza maumivu wakati mwanao anaota meno. Hata hivyo, mwone daktari wa watoto kabla jujampa mwanao dawa yoyote

Baada ya mwanao kuota meno hakikisha unayatunza vizuri


JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top