Related image
Ukuaji na maendeleo ya mtoto huanza tangu akiwa ndani ya mfuko wa uzazi na baada ya kuzaliwa hata anapofikia umri wa kubalehe.
Kwa kawaida mwili wa mtoto hukua vizuri endapo anapata chakula cha kutosha na chenye mjumuiko wa virutubisho vyote vinavyotakiwa kwa ukuaji wake na afya bora.

Ukuaji wa mtoto hutofautishwa na jinsi ambapo wataalamu wa afya wanasema maendeleo ya ukuaji wa mtoto wa kike ni tofauti na ukuaji wa mtoto wa kiume. Ukilinganisha maendeleo ya ukuaji wao mtoto wa kike hupata maendeleo ya kimwili mapeza zaidi kabla ya mtoto wa kiume.

Njia mojawapo rahisi inayotumiwa na wataalam wa afya na watu wengine kugundua mwenendo wa maendeleo ya ukuaji wa mtoto bila kujali jinsia huwa ni upimaji uzito.

Njia hii hutumika kwa kupima uzito na kulinganisha uzito huo na umri wa mtoto. Kwa kawaida mtoto mwenye afya njema hutakaiwa kuzaliwa akiwa na umri wa kilo 2.5 na 3.5 ambapo uzito huo huongezeka mara mbili baada ya miezi sita tangu kuzaliwa. Inakadiriwa kuwa mtoto mwenye umri wa miezi saba anatakiwa kuwa na uzito usiozidi kilo saba na anatakiwa kuwa na kilo 10 pale anapotimiza mwaka mmoja.

Maendeleo ya ukuaji wake inapaswa mtoto kutwa na kilo 12 anapotimiza miaka miwili, kilo 14 akiwa na miaka mitatu, kilo 16 akiwa na miaka minne na kilo 16 anapofikisha miaka mitano. Pia wataalamu hutumia urefu wa mwili wa mtoto kama kipimo cha maendeleo ya ukuaji wa mtoto chenye uhakika zaidi ya uzito kwani uzito unaweza kuathiriwa na mambo mengi kama upungufu wa maji mwilini ama mrundikano wa maji mwilini na magonjwa mengine yanayoweza kumpata mtoto.

Urefu wa mwili wa mtoto huwa na kasi zaidi katika miezi sita ya mwanzo ya maisha ya mtoto na huweza kukoma kwa muda na kushika kasi tena wakati mtoto anapofikia umri wa kubalehe. Kuota meno kwa mtoto ni hatua nyingine pia ya ukuaji wa mtoto ambapo meno huanza kuchomoza pale mtoto anapofikisha umri wa miezi sita.

Kwa kawaida mtoto huwa na meno 20 na inakadiriwa kuwa anapokuwa na umri wa miaka miwili hadi mitatu huota jino moja kila mwezi na meno ya kudumu huanza kuota mtoto anapofikisha umri wa miaka sita.

Njia nyingine inayotumika kujua ukuaji wa mtoto ni kipimo cha mzunguko wa mkono na mzunguko wa kichwa. Mtoto anapozaliwa na kuwa katika hali ya uchanga mzunguko wa kichwa chake huwa ni robo ya ukubwa wa mwili mzima na baadaye kadri anavyokuwa kichwa hukua na kufikia mzunguko wenye sentimeta 12 ndani ya miezi 12 tangu kuzaliwa ambapo sentimeta sita za urfu huu ni katika miezi mitatu ya kwanza, sentimeta tatu nyingine kwa miezi mtatu inayofuatia na sentimeta tatu tena kwa miezi mitatu iliyobaki.

Mtoto wa chini ya mwaka mmoja mzunguko wa kichwa chake huwa mkubwa kuliko mzunguko wa kifua chake na ukimlinganisha na Yule mwenye umri zaidi ya mwaka mmoja. Pia mzunguko wa sehemu ya kati ya mkono wa mtoto huongezeka kwa haraka zaidi na kufikia sentimeta 16 ambapo husimama na kutobadilika mtoto anapokuwa na umri wa mwaka mmoja mpaka miaka mitano.

Baada ya miaka mitano mzunguko wa mkono huweza kuongezeka kwa sentimeta moja mpaka 17. 

Huduma za maendeleo ya ukuaji wa mtoto hupatikana na kufanyika katika kliniki za watoto na mahospitalini kote, hivyo ni vizuri wazazi kuhakikisha kuwa wanafika katika maeneo hayo ili kujua maendeleo ya ukuaji wa watoto wao.

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top