Na :MARTHA MAGAWA
Related image
Penzi la aina ya tatu linalotajwa na watafiti ni lile lijulikanalo kama penzi la Uigizaji. Hili ni lile penzi ambalo wanaopendana hukutana asubuhi na ikifika jioni tayari ni wapenzi kamili, ambapo hugandamana kama ruba, utadhani waigizaji wako kwenye matayarisho ya filamu.

Ukiwatazama wanakuwa kama vichaa na msukumo wao wa kutimiza hisia za mwili huwa ni mkubwa kiasi cha kufikia kufanya mapenzi hata barabarani au kwenye sehemu za wazi. Wapenzi wa aina hii huchukua muda mfupi sana kutangaziana mambo ya ndoa na pengine kuoana bila kufahamiana zaidi kitabia. Wanajuana asubuhi na jioni mwanamke /mwanaume keshahamia kwa mwenzake na maisha yanaanza, hapo hakuna ushauri wala muongozo wa watu wengine.
Related image
Tatizo kubwa ambalo hujitokeza katika penzi la aina hii ni wapenzi kuchokana mapema na hamu ya kufanya tendo la ndoa kupotea. “Yaani nikiwa na mume wangu sijisikii kabisa kufanya naye mapenzi, lakini kwa wengine nakuwa na hamu sana” hizi ni kauli za wapenzi wa penzi la kisinema sinema.

Mbali na hilo wapenzi wa aina hii ni rahisi kuporwa na kuanzisha uhusiano mpya, hivyo inashauriwa kuwa kwa wale ambao wanaona kuwa wako kwenye kundi hili, wajitahidi kujizuia na kupeana nafasi za kujuana zaidi kupitia ushauri wa watu wengine.


Si vema kushiriki tendo la ndoa kila mara kwa staili na sehemu zile zile na pia haifai kukurupuka kuoana bila kuchunguzana tabia, ndoa za hivi hazidumu.

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top