Hakuna
mtu ambaye ameshawahi kuishi bila kusema uongo kabisa.. kitaalamu mtu akiulizwa
swali akajibu uongo, hali ya mwili hubadilika yaani mapigo ya moyo hukimbia,
presha hupanda na anaweza hata kutokwa jasho. Kuna kipimo cha polygraphy ambaho
hutumia njia hii kufahamu kama mtu anadanganya au vipi kwa kuangalia mabadiliko
ya mfumo wa mwili pale anapokua anaulizwa maswali, mara nyingi kipimo cha
polygraphy hutumika na askari polisi
Sasa
leo nitakujuza jinsi ya kujua mtu, rafiki yako, ndugu yako, mpenzi wako kama anakudanganya
kwa kuangalia vitu muhimu wakati wa kumohoji.
Kitu cha kwanza ni kuchelewa
kujibu swali;
yaan
ukimuuliza mtu swali akachelewa kujibu kuna uwezekano mkubwa anadanganya lakini
inategemea na aina ya swali ulilolo muuliza.
Pili ni kukosekana
mahusiano ya maneno na vitendo;
kwa
hali ya kawaida mtu akiulizwa swali na akatakiwa kujibu ndio au hapana kama ni
ndio atatikisa kichwa kwenda juu na kama sio kweli atatikisa kichwa kwa pembeni
sasa mtu akiulizwa swali akadanganya ataenda tofauti na hali ya kawaida hapo
utaona kwamba ulimi wake unakubali lakini mwili wake umekataa.
Tatu ni kukohoa kidogo au
kumeza kabla ya kujibu;
mtu
akipata wasiwasi baada ya kuulizwa kitu ambacho kimemkosesha amani kitaalamu
mfumo wa mishipa ya fahamu kama sympathetic
pathway
unakua umefanya kazi hivyo mate yatakauka mdomoni na kwenye koo hivyo kuondoa
hiyo hali atakohoa kidogo au kumeza mate kabla hajajibu ili kupata muda zaidi
wa kutafuta cha kudanganya.
Nne ni kuficha macho au
mdomo kwa kutumia mikono;
hii
hutokea bila yeye kufahamu kitaalamu kama subconcious level yaani kibinadamu anashindwa kuuvumilia ule uongo anaosema
hivyo atajikuta mwenyewe anaweka mikono sehemu hizo bila kujua ila wewe
unayemuuliza maswali ndio utagundua kwamba anadanganya.
Tano ni kushika shika sana
sehemu za kichwa chake;
mfumo
wa sympathetic system ukianza kufanya kazi
mishipa ya damu huanza kujikunja hasa na sehemu zinazokosa damu kama usoni
huanza kuwasha kwa mbali na kua tofauti hivyo muongo atajikuta anakuna pua,
anakuna sikio na hata viganja vya mikono.
Sita ni kuhangaika
mazingira yanayomzunguka;
mtu
anayedanganya akiulizwa swali anaweza kuanza kuanza kurekebisha vitu ambavyo
viko sahihi kwa mfano kurekebisha tai,miwani, kuchomekea vizuri...
kama
ni mwanamke muongo ataanza kuweka nywele vizuri na kurekebisha sketi yake kabla
ya kujibu kumbuka kama akifanya vitu hivyo baada ya kujibu sio muongo au
unamuuliza mtu swali amekaa mezani ghafla kila kitu kimebadilika sehemu
kilipokuwepo yaani kahamisha glass ya maji, funguo zake, simu na kadhalika.
Saba ni kushindwa
kukuangalia usoni;
Unaweza
ukaanza kumuuliza vitu vya kweli kabisa huku mnaangaliana lakini ghafla chomeka
swali la tofauti ambalo unataka kujua kama ni kweli au sio kweli basi utaona
anaanza kungalia pembeni na kushidwa kuangalia usoni na wakati mwingine kijasho
chembamba kitamtoka.
Lakini nane ni kua na
maneno mengi sana;
unaweza
ukampigia simu ukamuuliza mtu kwamba yuko wapi akakujibu nilienda hospitali
kuona mgonjwa nimechoka sana ntajitahidi leo nilale mapema nk... mtu wa huyu anaweza kua medanganya kitu sasa
anajaribu kukificha na maneno mengi ili usimjue lakini ukute kwa hali ya
kawaida angesema niko hospitali kisha akakaa kimya.
Tisa ni kupunguza
sauti;
mtu
kama ukianza kumuuliza mambo anayofahamu
kwa uhakika mfano jina lake, miaka yake, anaishi wapi au kama ni mchumba wako
unaweza kumuuliza rafiki yake anaitwa nani, anafanya kazi gani na hapo atakua
mchangamfu na kujibu vizuri kisha ghafla ukamuuliza nasikia umelala na mwanaume
fulani hapo sauti itakua ndogo na atakataa kwa sauti ya chini.
Mwisho kabisa ni kuapa
mara nyingi;
Mtu
muongo hujitahidi sana kujitetea aonekane hana kosa yaani kila baada ya muda
ata apa kwa mungu, atakua na kauli kama 'ukweli kutoka moyoni".
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv