Image result for Jinsi ya kukabiliana na  msongo wa mawazo stress
Kwanza Msongo wa mawazo unaweza kukufanya ushindwe kufanya shughuli zako za kila siku kwa ufanisi. lakini  msongo wa mawazo unaepukika, kivipi.............

1. Usiweke Malengo ambayo Hayafikiki
Kila mtu ana uwezo na vipawa vyake tofauti na mtu mwingine, unapoweka malengo yako hakikisha unazingatia uwezo, vipawa na muda ulionao ili kuweza kuyafanikisha. Usiweke malengo sababu watu wengine wameweka hayo,au ukaweka muda kiasi fulani sababu watu wote wameweka hivyo, daima zingatia uwezo wako ili malengo yako yaweze kufanikiwa na kuepuka kupata stress'.
Image result for Jinsi ya kukabiliana na  msongo wa mawazo stress
2. Jifunze Kukubali Changamoto
Jifunze kukabili changamoto na sio kusikitika kwa nini mambo hayajawa kama ulivyotaka na kubaki ukisononeka. Jaribu kukubali mambo kwa busara zaidi, na utulivu huku ukitafakari nini cha kufanya ili kulipata lile ulilo kusudia. Changamoto iwe ni chachu ya wewe kuzidi kukazana na kujaribu zaidi.

3. Fanya Maamuzi Pale Unapopaswa
unatakiwa Uwe na ujasiri wa kuamua mara baada ya kutafakari pande zote kwa makini na kuona faida na hasara za kila upande. Usihofu sana juu ya kuweza kufanya makosa hadi ukaishia kupata msongo wa mawazo, mara nyingine watu hujifunza kutokana na makosa.
Image result for Jinsi ya kukabiliana na  msongo wa mawazo stress
4. Kuwa na Mipango
Kutokuwa na mipango ni sababu moja kubwa sana inayoweza kukuletea msongo wa mawazo.

5. Usiweke Jambo Linalokusumbua Moyoni
Jifunze kutokuweka mambo yanayokuumiza moyoni maana katika hali hiyo ni rahisi sana kupata msongo wa mawazo. Uwe na tabia ya kupeleka wasiwasi na hofu zako zote mbele za Mungu kwa maombi na pia kuongea na mtu ambaye unajua atakuwa msaada kwako.

6. Jali Mwili Wako
Ni muhimu sana mwili wako uwe katika hali nzuri na afya bora ili uweze kufanya kazi zako vizuri na kwa wepesi. Hakikisha unakula chakula chenye virutubisho bora na pia unakunywa maji ya kutosha. Fanya mazoezi ya viungo mara kwa mara na pata muda wa kutosha wa kupumzika kila siku.
Related image
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top