Ukuaji na maendeleo ya mtoto huanza tangu akiwa
ndani ya mfuko wa uzazi na baada ya kuzaliwa hata anapofikia umri wa kubalehe.
Kwa kawaida mwili wa mtoto hukua vizuri endapo
anapata chakula cha kutosha na chenye mjumuiko wa virutubisho vyote
vinavyotakiwa kwa ukuaji wake na afya bora.
Ukuaji wa mtoto hutofautishwa na jinsi ambapo
wataalamu wa afya wanasema maendeleo ya ukuaji wa mtoto wa kike ni tofauti na
ukuaji wa mtoto wa kiume. Ukilinganisha maendeleo ya ukuaji wao mtoto wa kike
hupata maendeleo ya kimwili mapeza zaidi kabla ya mtoto wa kiume.
Njia mojawapo rahisi inayotumiwa na wataalam wa afya
na watu wengine kugundua mwenendo wa maendeleo ya ukuaji wa mtoto bila kujali
jinsia huwa ni upimaji uzito.
Njia hii hutumika kwa kupima uzito na kulinganisha
uzito huo na umri wa mtoto. Kwa kawaida mtoto mwenye afya njema hutakaiwa
kuzaliwa akiwa na umri wa kilo 2.5 na 3.5 ambapo uzito huo huongezeka mara
mbili baada ya miezi sita tangu kuzaliwa. Inakadiriwa kuwa mtoto mwenye umri wa
miezi saba anatakiwa kuwa na uzito usiozidi kilo saba na anatakiwa kuwa na kilo
10 pale anapotimiza mwaka mmoja.
Maendeleo ya ukuaji wake inapaswa mtoto kutwa na
kilo 12 anapotimiza miaka miwili, kilo 14 akiwa na miaka mitatu, kilo 16 akiwa
na miaka minne na kilo 16 anapofikisha miaka mitano. Pia wataalamu hutumia
urefu wa mwili wa mtoto kama kipimo cha maendeleo ya ukuaji wa mtoto chenye
uhakika zaidi ya uzito kwani uzito unaweza kuathiriwa na mambo mengi kama
upungufu wa maji mwilini ama mrundikano wa maji mwilini na magonjwa mengine
yanayoweza kumpata mtoto.
Urefu wa mwili wa mtoto huwa na kasi zaidi katika
miezi sita ya mwanzo ya maisha ya mtoto na huweza kukoma kwa muda na kushika
kasi tena wakati mtoto anapofikia umri wa kubalehe. Kuota meno kwa mtoto ni
hatua nyingine pia ya ukuaji wa mtoto ambapo meno huanza kuchomoza pale mtoto
anapofikisha umri wa miezi sita.
Kwa kawaida mtoto huwa na meno 20 na inakadiriwa
kuwa anapokuwa na umri wa miaka miwili hadi mitatu huota jino moja kila mwezi
na meno ya kudumu huanza kuota mtoto anapofikisha umri wa miaka sita.
Njia nyingine inayotumika kujua ukuaji wa mtoto ni
kipimo cha mzunguko wa mkono na mzunguko wa kichwa. Mtoto anapozaliwa na kuwa
katika hali ya uchanga mzunguko wa kichwa chake huwa ni robo ya ukubwa wa mwili
mzima na baadaye kadri anavyokuwa kichwa hukua na kufikia mzunguko wenye
sentimeta 12 ndani ya miezi 12 tangu kuzaliwa ambapo sentimeta sita za urfu huu
ni katika miezi mitatu ya kwanza, sentimeta tatu nyingine kwa miezi mtatu inayofuatia
na sentimeta tatu tena kwa miezi mitatu iliyobaki.
Mtoto wa chini ya mwaka mmoja mzunguko wa kichwa
chake huwa mkubwa kuliko mzunguko wa kifua chake na ukimlinganisha na Yule
mwenye umri zaidi ya mwaka mmoja. Pia mzunguko wa sehemu ya kati ya mkono wa
mtoto huongezeka kwa haraka zaidi na kufikia sentimeta 16 ambapo husimama na
kutobadilika mtoto anapokuwa na umri wa mwaka mmoja mpaka miaka mitano.
Baada ya miaka mitano mzunguko wa mkono huweza
kuongezeka kwa sentimeta moja mpaka 17.
Huduma za maendeleo ya ukuaji wa mtoto
hupatikana na kufanyika katika kliniki za watoto na mahospitalini kote, hivyo
ni vizuri wazazi kuhakikisha kuwa wanafika katika maeneo hayo ili kujua
maendeleo ya ukuaji wa watoto wao.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv