Related image
Mara nyingi Kujiandaa kwa interview ni kazi nzito kwa watafuta ajira wengi unaweza kujiuliza unaanzia wapi? Una tazamiaje maswali atakayokuuliza mwajiri?
Unajibuje maswali ya interview?
Wasiwasi wa kuwaza interview insababisha watu wengi kuwa na hofu na hivyo kumfanya afanye kosa kubwa kabis, kuongea bila mpangilio.
Njia moja ya kuzuia hii kutokea ni kufuatilia mfumo wa kujibu maswali.
Kwanza, toa mfano wa kazi uliyofanya na jinsi gani ilikusaidia kutatua tatizo linalo kumba hiyo kampuni hivi sasa. Kwa mfano, “kwenye ofisi yangu ya zamani, nilikuwa na changamoto  Fulani kilichokuwaa na matatizo zinazofanana na hii.”
Baada ya hapo, elezea hatua ulizochukua kutatua tatizo hili.
Malizia kuelezea matokeo yake na jinsi gani ulichojifunza kwa kupitia hayo kitasaidia kampuni hiyo na changamoto zake.
Image result for Interview
Sasa  unajua namna ya kujibu maswali, ujiandae na maswali yapi?
1. Tupe maelezo mafupi kuhusu wewe
Hapa, mwajiri hataki kujua kuhusu maisha yako binafsi, familia yako au unachopenda kufanya nje ya kazini. Mwajiri anataka umueleze kwa ufupi kuhusu kazi ulizofanya. Ulifikaje hapa na unataka kufika wapi.
Sasa wewe  andaa maelezo ya kazi ulizofanya isiyozidi sekunde 30 na jinsi gani kazi hizi zimekuandaa kwa nafasi hii.
2. Kwa nini tukuajiri?
Kama unataka kubaki kwenye fikra za mwajiri zaidi ya wengine, usiwape orodha ya sifa zako – mwajiri anazijua tayari kupitia CV yako. Badala yake, waambie utawasaidiaje kutatua matatizo na changamoto zao. Kutoa jibu kamilifu hapa, waeleze ni jinsi gani utwasaidia wao badala a jinsi gani watakusaidia wewe.
3. Sifa yako kubwa ni nini?
Hii ni nafasi yako kuelezea sifa ulionayo ambayo unajua ni muhimu kwa kampuni hiyo na nafasi hiyo unayoitaka. Ila, usifanye kosa la kusema “mimi ni hodari kwa kuwasiliana”. Badala yake, toa maelezo kwa kuhadithia.
4. Upungufu wako mkubwa ni nini?
Hapa, waajiri wanataka kuona kama unajijua, kama unaweza kukubali kwamba una mapungufu na zaidi ya hapo, kama uko tayari kuzifanyia kazi.
Sasa wewe fikiria pungufu ambalo halina umuhimu mkubwa kwa kazi hiyo alafu ongelea hatua ulizochukua au utakazochukua kujiboresha hapo.
Usiseme kwamba huna pungufu lolote. Kila mtu anapungufu au mapungufu.
5. Kwa nini unataka kufanya kazi hapa?
Hili swali pia halihusu jinsi gani kampuni itakusaidia wewe ila, jinsi gani utakuwa faida kwao.
Utafiti juu ya kampuni utakaokuwa umefanya ulivyokuwa unaandaa CV na barua ya kuomba kazi itakusaidia hapa. Fikiria jinsi gani nafasi hiyo unayotaka itasaidia kampuni na kwa nini una nia ya kufanya kazi hapo.
Waajiri wanatafuta watu wenye hamu ya kufanya kazi kwao na sio kwamba ni mtu anayetafuta ajira tu. Wanatafuta watu wenye shauku na mawazo. Huu ni muda wako wakuonyesha mawazo yako.
6. Kwa nini uliacha kazi pale ulipokuwa?
Usimseme vibaya mwajiri wala wafanyakazi wako wa zamani. Badala yake, sema tu kwamba unatafuta “changamoto mpya ya kikazi”, ila eleza zaidi kwa kuwaambia jinsi gani kazi hii itakupa changamoto ulizokosa kwenye kazi uliyoacha.
7. Unatarajia kupata nini kutokana na kufanya kazi hapa?
Ongelea unachotumaini kutimiza ila kuwa mkweli. Pia usiongee kwa ujumla. Chagua kitu maalum ambalo ni muhimu kwa kampuni alafu ilenge. Ila, uwe wazi kwa kusema itachukua muda kujifunza zaidi kuhusu kampuni ili kufanikiwa zaidi.
8. Toa mfano ya tatizo ulilokumbwa nayo na ulichofanya kulitatua
Mradi umejiandaa kujibu hii swali, halitakupa shida. Chaguo mfano unaoonyesha ujuzi muhimu inayohitajika kwa kazi hii.
9. Unatarajia kupata mshaara wa kiasi gani?
Hakikisha unafanya utafiti juu ya viwango vya mishaara kwa nafasi hiyo na kwamba umeshafikiria hili. Ingia na viwango viwili, ya chini iwe unayoweza kukubali na ya juu iwe unayopenda.
Usipojiandaa na ukajaribu kuhisia, unaweza ukaishia kujionea.
10. Una maswali yoyote ya kutuuliza?
Mwishoni wa interview, ni kawaida kwa mwajiri kuuliza kama una maswali kwao. Ukipewa nafasi hii, usiulizie mshaara na faida zingine. Badala yake, uliza:
·   Maadili ya kampuni
·   Aina ya uongozi
·   Wafanyakazi wenzako
·   Chochote ambacho hukuelewa kuhusu kazi hiyo.
·   Watakupa jibu baada ya muda gani?
Image result for Interview
maswali ya ziada:
Baada ya miaka 5, unataka uwe umefikia wapi?
Mwajiri atakuuliza hili swali kujua kama utafuta ajira tu kupata mshaara au kama kweli unataka hii kazi kwa sababu umeipenda na inaendana na malengo yako ya kazi. Kwa hiyo, kwa kuwa wengi wetu hatujui kwa uhakika ni wapi tutakapofikia baada miaka 5, jaribu kufikiria hilo.
Tiba bora ya msongo wa interview ni kujiandaa
Ingawa interview inaweza ikakupa misongo mingi, ukijiandaa vizuri, kama chochote maishani. Utashangazwa na mafanikio yako.
Interview ni nafasi yako ya mwisho kumvutia mwajiri, na vidokezo vilivyoelezwa hapo juu zitakusaidia na hilo.
hamna haja ya kuwa na wasiwasi ukiwa umejiandaa.

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv

 
Top