Image result for Kuandika CV(wasifu)
Zaidi ya asilimia 10 ya watu nchini wamekosa ajira na makampuni hupokea wastani wa maombi 100 ya kazi kwa tangazo moja la kazi. Hivyo, CV yako lazima ijitokeze vizuri. Utaratibu wa kuomba kazi inaweza ikawa tofauti kati ya makampuni na mashirika, ila yote yatahitaji uwatumie CV.
Hebu leo tujifunze siri za kuandika cv
Image result for Kuandika CV(wasifu)
kwanza CV ni nini?
CV ni maelezo ya ujumla kwa undani ya historia yako ya kazi na shule. Kawaida, inatumika kwenye maombi ya kazi ya nafasi za kati, za juu na za utafiti.
vifuatayo ni vidokezo vitakavyokusaidia kufanya CV yako iwe bora na kukusaidia kupata interview.
Kuwa na mpango
Kabla ya kuiandika inabidi ufanye vifuatayo:
1.    Soma na kuelewa maelezo ya kazi
Una ujuzi gani? Mwajiri anatafuta mfanyakazi wa aina gani? Maswali haya ni muhimu kujua kama utaiweza hiyo kazi au la. Pia, ni vizuri kujua nini hasa ni muhimu kwa muajiri na kufanya maombi yako yaendane zaidi na mahitaji ya mwajiri.
2.    Andika maneno muhimu yaliyotumika kwenye maelezo ya kazi, uzitumie kwenye CV
Usichuke sentensi nzima kutoka kwenye maelezo ya kazi na ukaitumia vile vile kwenye CV yako. Ila, tumia lugha na baadhi ya maneno yaliyotumika kwenye CV.
3.    Fanya utafiti juu ya kampuni iliyotangaza kazi
Pamoja na kuchambua maelezo ya kazi, ni muhimu kufanya utafiti juu ya kampuni yenyewe. Kama wana tovuti au wapo kwenye mitandao ya kijamii, jaribu kujua ni kazi gani na sekta ipi wanayohusika nayo. Pia, ikiwezekana jaribu kuwajua wafanyakazi/meneja wa kampuni hiyo. Hii itakusaidia kujua maadili na muelekeo wa kampuni. Hii itakusaidia kuweka maombi yako ya kazi yaendane na kampuni hiyo.
4.    Orodhesha ujuzi wako wakufanya kazi
Hapa, usiweke kazi zote ulizozifanya maishani mwako ila, weka zile ambazo zilikuongezea ujuzi utakayo kusaidia kufanya kazi unayoomba.
Andika
Staili inayotumika zaidi kwenye kuandika CV ni ifuatayo:
1.    Lengo la CV na ujuzi wako
2.    Ujuzi wako wa kazi
3.    Mafanikio maalum
4.    Elimu
5.    Ujuzi muhimu binafsi
Business Insider wanasema kwamba kwa wastani, mwajiri anaangalia CV kwa sekunde 6 tu kabla ya kuamua kama mtafuta ajira anafaa au hafai. Kwa hiyo, hakikisha kwamba:
1 – Zingatia staili
·   Tumia maandishi ya kawaida ya Times New Roman
·   Tumia size 9 – 12 ya herufi
·   Hakikisha unatumia staili moja ya kuandaa CV kote
2 – Hakikisha ni rahisi kusoma na kuelewa
·   CV isiwe zaidi ya ukursasa 2
·   Usitumie sentensi ndefu
Fikiria msomaji
Hakikisha CV yako inasomeka kiurahisi na inawasilisha mafanikio yako kwa uwazi.
Tumia maneno yanayonyesha matendo
Maneno yanayo onyesha matendo yanaonyesha kwamba wewe ni mtu wa matendo, mchapa kazi. Maneno ya aina hii ni kama:
·   Kusimamia
·   Kupata
·   Kuchambua
·   Kusuluhisha
·   Kuboresha
·   Kufanya
Lengo la kutumia maneno kama haya nikuonyesha uwezo na faida yako ndani ya mazingira ya kufanya kazi. Mwajiri anabidi auone mchango wako wa kikazi.
Anza na kazi yako ya sasa hivi au ya hivi karibuni alafu rudi nyuma. Hakikisha una:
Ukiwa unaandika jina la kampuni uliyo fanya kazi, andika jina la kampuni kikamilifu. Pili, eleza kwa ufupi kampuni yao inahusika na nini. Tatu, weka muda uliyofanyakazi hapo (mwezi na mwaka). Baada ya hapo, orodhesha kazi na majukumu lako kwenye hilo kampuni.
Tumia nambari asilimia popote panapo faa
Kwa mfano, badala ya kuandika ‘nilichangia ongezeko la mauzo ya kampuni’ andika, ‘nilichangia ongezeko la mauzo ya kampuni kwa 25%’
Usidanganye
Hii ni tatizo kubwa sana Tanzania na ukidanganya, utagundulika tu na mwajiri akifanya utafiti wake juu yako. Ni sababu kubwa sana ya mtu kukosa ajira.
Image result for Kuandika CV(wasifu)
Mwisho
1.    Pitia kila kitu kwa mara ya mwisho
Makosa ya sarufi au ya kuandika maneno kadhaa yanaweza kusababishe ukose ajira kwa kuwa yanonyesha kwamba hauko makini na kazi yako.
Dokezo la ziada: Print CV yako alafu ipitie. Hii huwa inasaidia kuona makosea yako.
2.    Rafiki apitie CV
Muombe rafiki yako apitie CV yako. Macho manne ni bora zaidi ya mawili!
Hatua ya kwanza kwenye kupata kazi unayotaka ni kutuma maombi. Tunatumaini kwamba vidokezo vilivyo elezwa humu zitakusaidia kuandaa CV bora kwa ajili ya mwajiri.
Image result for Kuandika CV(wasifu)

 JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv

 
Top