Mara nyingi Kujiandaa kwa interview ni kazi nzito kwa watafuta ajira wengi
unaweza kujiuliza unaanzia wapi? Una tazamiaje maswali atakayokuuliza mwajiri?
Unajibuje maswali ya
interview?
Wasiwasi wa kuwaza interview
insababisha watu wengi kuwa na hofu na hivyo kumfanya afanye kosa kubwa kabis,
kuongea bila mpangilio.
Njia moja ya kuzuia hii
kutokea ni kufuatilia mfumo wa kujibu maswali.
Kwanza, toa mfano wa kazi uliyofanya na jinsi gani
ilikusaidia kutatua tatizo linalo kumba hiyo kampuni hivi sasa. Kwa
mfano, “kwenye ofisi yangu ya zamani, nilikuwa na
changamoto Fulani kilichokuwaa na
matatizo zinazofanana na hii.”
Baada ya hapo, elezea hatua
ulizochukua kutatua tatizo hili.
Malizia kuelezea matokeo
yake na jinsi gani ulichojifunza kwa kupitia hayo kitasaidia kampuni hiyo na
changamoto zake.
Sasa unajua namna ya kujibu maswali, ujiandae na
maswali yapi?
1. Tupe maelezo mafupi
kuhusu wewe
Hapa, mwajiri hataki kujua
kuhusu maisha yako binafsi, familia yako au unachopenda kufanya nje ya kazini.
Mwajiri anataka umueleze kwa ufupi kuhusu kazi ulizofanya. Ulifikaje hapa na
unataka kufika wapi.
Sasa wewe andaa maelezo ya kazi ulizofanya isiyozidi
sekunde 30 na jinsi gani kazi hizi zimekuandaa kwa nafasi hii.
2. Kwa nini tukuajiri?
Kama unataka kubaki kwenye
fikra za mwajiri zaidi ya wengine, usiwape orodha ya sifa zako – mwajiri
anazijua tayari kupitia CV yako. Badala yake, waambie utawasaidiaje kutatua
matatizo na changamoto zao. Kutoa jibu kamilifu hapa, waeleze ni jinsi gani
utwasaidia wao badala a jinsi gani watakusaidia wewe.
3. Sifa yako kubwa ni nini?
Hii ni nafasi yako kuelezea
sifa ulionayo ambayo unajua ni muhimu kwa kampuni hiyo na nafasi hiyo
unayoitaka. Ila, usifanye kosa la kusema “mimi
ni hodari kwa kuwasiliana”. Badala yake, toa maelezo kwa kuhadithia.
4. Upungufu wako mkubwa ni
nini?
Hapa, waajiri wanataka
kuona kama unajijua, kama unaweza kukubali kwamba una mapungufu na zaidi ya
hapo, kama uko tayari kuzifanyia kazi.
Sasa wewe fikiria pungufu ambalo halina umuhimu mkubwa
kwa kazi hiyo alafu ongelea hatua ulizochukua au utakazochukua kujiboresha
hapo.
Usiseme
kwamba huna pungufu lolote. Kila mtu anapungufu au mapungufu.
5. Kwa nini unataka kufanya
kazi hapa?
Hili swali pia halihusu
jinsi gani kampuni itakusaidia wewe ila, jinsi gani utakuwa faida kwao.
Utafiti juu ya kampuni
utakaokuwa umefanya ulivyokuwa unaandaa CV na barua ya kuomba kazi itakusaidia
hapa. Fikiria jinsi gani nafasi hiyo unayotaka itasaidia kampuni na kwa nini
una nia ya kufanya kazi hapo.
Waajiri wanatafuta watu
wenye hamu ya kufanya kazi kwao na sio kwamba ni mtu anayetafuta ajira tu.
Wanatafuta watu wenye shauku na mawazo. Huu ni muda wako wakuonyesha mawazo
yako.
6. Kwa nini uliacha kazi
pale ulipokuwa?
Usimseme vibaya mwajiri
wala wafanyakazi wako wa zamani. Badala yake, sema tu kwamba unatafuta “changamoto
mpya ya kikazi”,
ila eleza zaidi kwa kuwaambia jinsi gani kazi hii itakupa changamoto ulizokosa
kwenye kazi uliyoacha.
7. Unatarajia kupata nini
kutokana na kufanya kazi hapa?
Ongelea unachotumaini
kutimiza ila kuwa mkweli. Pia usiongee kwa ujumla. Chagua kitu maalum ambalo ni
muhimu kwa kampuni alafu ilenge. Ila, uwe wazi kwa kusema itachukua muda
kujifunza zaidi kuhusu kampuni ili kufanikiwa zaidi.
8. Toa mfano ya tatizo
ulilokumbwa nayo na ulichofanya kulitatua
Mradi umejiandaa kujibu hii
swali, halitakupa shida. Chaguo mfano unaoonyesha ujuzi muhimu inayohitajika
kwa kazi hii.
9. Unatarajia kupata
mshaara wa kiasi gani?
Hakikisha unafanya utafiti
juu ya viwango vya mishaara kwa nafasi hiyo na kwamba umeshafikiria hili. Ingia
na viwango viwili, ya chini iwe unayoweza kukubali na ya juu iwe unayopenda.
Usipojiandaa
na ukajaribu kuhisia, unaweza ukaishia kujionea.
10. Una maswali yoyote ya
kutuuliza?
Mwishoni wa interview, ni
kawaida kwa mwajiri kuuliza kama una maswali kwao. Ukipewa nafasi hii,
usiulizie mshaara na faida zingine. Badala yake, uliza:
·
Maadili ya kampuni
·
Aina ya uongozi
·
Wafanyakazi wenzako
·
Chochote ambacho hukuelewa kuhusu kazi hiyo.
·
Watakupa jibu baada ya muda gani?
maswali ya ziada:
Baada ya miaka 5, unataka
uwe umefikia wapi?
Mwajiri atakuuliza hili
swali kujua kama utafuta ajira tu kupata mshaara au kama kweli unataka hii kazi
kwa sababu umeipenda na inaendana na malengo yako ya kazi. Kwa hiyo, kwa kuwa
wengi wetu hatujui kwa uhakika ni wapi tutakapofikia baada miaka 5, jaribu
kufikiria hilo.
Tiba bora ya msongo wa
interview ni kujiandaa
Ingawa interview inaweza
ikakupa misongo mingi, ukijiandaa vizuri, kama chochote maishani. Utashangazwa
na mafanikio yako.
Interview ni nafasi yako ya
mwisho kumvutia mwajiri, na vidokezo vilivyoelezwa hapo juu zitakusaidia na
hilo.
hamna
haja ya kuwa na wasiwasi ukiwa umejiandaa.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW