Zaidi ya asilimia 10 ya
watu nchini wamekosa ajira na makampuni hupokea wastani wa maombi 100 ya kazi
kwa tangazo moja la kazi. Hivyo, CV yako lazima ijitokeze vizuri. Utaratibu wa
kuomba kazi inaweza ikawa tofauti kati ya makampuni na mashirika, ila yote
yatahitaji uwatumie CV.
Hebu leo tujifunze siri za
kuandika cv
kwanza CV ni nini?
CV ni maelezo ya ujumla kwa undani ya historia yako
ya kazi na shule. Kawaida, inatumika kwenye maombi ya kazi ya nafasi za
kati, za juu na za utafiti.
vifuatayo ni vidokezo vitakavyokusaidia
kufanya CV yako iwe bora na kukusaidia kupata interview.
Kuwa na mpango
Kabla ya kuiandika inabidi
ufanye vifuatayo:
1. Soma na kuelewa maelezo ya kazi
Una ujuzi gani? Mwajiri
anatafuta mfanyakazi wa aina gani? Maswali haya ni muhimu kujua kama utaiweza
hiyo kazi au la. Pia, ni vizuri kujua nini hasa ni muhimu kwa muajiri na
kufanya maombi yako yaendane zaidi na mahitaji ya mwajiri.
2. Andika maneno muhimu yaliyotumika kwenye maelezo ya kazi,
uzitumie kwenye CV
Usichuke sentensi nzima
kutoka kwenye maelezo ya kazi na ukaitumia vile vile kwenye CV yako. Ila, tumia
lugha na baadhi ya maneno yaliyotumika kwenye CV.
3. Fanya utafiti juu ya kampuni iliyotangaza kazi
Pamoja na kuchambua maelezo
ya kazi, ni muhimu kufanya utafiti juu ya kampuni yenyewe. Kama wana tovuti au
wapo kwenye mitandao ya kijamii, jaribu kujua ni kazi gani na sekta ipi
wanayohusika nayo. Pia, ikiwezekana jaribu kuwajua wafanyakazi/meneja wa
kampuni hiyo. Hii itakusaidia kujua maadili na muelekeo wa kampuni. Hii
itakusaidia kuweka maombi yako ya kazi yaendane na kampuni hiyo.
4. Orodhesha ujuzi wako wakufanya kazi
Hapa, usiweke kazi zote
ulizozifanya maishani mwako ila, weka zile ambazo zilikuongezea ujuzi utakayo
kusaidia kufanya kazi unayoomba.
Andika
Staili inayotumika zaidi
kwenye kuandika CV ni ifuatayo:
1. Lengo la CV na ujuzi wako
2. Ujuzi wako wa kazi
3. Mafanikio maalum
4. Elimu
5. Ujuzi muhimu binafsi
Business Insider wanasema kwamba kwa wastani, mwajiri
anaangalia CV kwa sekunde 6 tu kabla ya kuamua kama mtafuta ajira anafaa au
hafai. Kwa hiyo, hakikisha kwamba:
1 – Zingatia staili
·
Tumia
maandishi ya kawaida ya Times New Roman
·
Tumia
size 9 – 12 ya herufi
·
Hakikisha
unatumia staili moja ya kuandaa CV kote
2 – Hakikisha ni rahisi
kusoma na kuelewa
·
CV
isiwe zaidi ya ukursasa 2
·
Usitumie
sentensi ndefu
Fikiria msomaji
Hakikisha CV yako inasomeka
kiurahisi na inawasilisha mafanikio yako kwa uwazi.
Tumia maneno yanayonyesha
matendo
Maneno yanayo onyesha
matendo yanaonyesha kwamba wewe ni mtu wa matendo, mchapa kazi. Maneno ya aina
hii ni kama:
·
Kusimamia
·
Kupata
·
Kuchambua
·
Kusuluhisha
·
Kuboresha
·
Kufanya
Lengo la kutumia maneno
kama haya nikuonyesha uwezo na faida yako ndani ya mazingira ya kufanya kazi.
Mwajiri anabidi auone mchango wako wa kikazi.
Anza na kazi yako ya sasa hivi au ya hivi karibuni alafu
rudi nyuma. Hakikisha una:
Ukiwa unaandika jina la kampuni
uliyo fanya kazi, andika jina la kampuni kikamilifu. Pili, eleza kwa ufupi
kampuni yao inahusika na nini. Tatu, weka muda uliyofanyakazi hapo (mwezi na
mwaka). Baada ya hapo, orodhesha kazi na majukumu lako kwenye hilo kampuni.
Tumia nambari asilimia
popote panapo faa
Kwa mfano, badala ya
kuandika ‘nilichangia ongezeko la mauzo ya kampuni’ andika, ‘nilichangia
ongezeko la mauzo ya kampuni kwa 25%’
Usidanganye
Hii ni tatizo kubwa sana
Tanzania na ukidanganya, utagundulika tu na mwajiri akifanya utafiti wake juu
yako. Ni sababu kubwa sana ya mtu kukosa ajira.
Mwisho
1. Pitia kila kitu kwa mara ya
mwisho
Makosa ya sarufi au ya
kuandika maneno kadhaa yanaweza kusababishe ukose ajira kwa kuwa yanonyesha
kwamba hauko makini na kazi yako.
Dokezo la ziada: Print CV yako alafu ipitie.
Hii huwa inasaidia kuona makosea yako.
2. Rafiki apitie CV
Muombe rafiki yako apitie
CV yako. Macho manne ni bora zaidi ya mawili!
Hatua ya kwanza kwenye
kupata kazi unayotaka ni kutuma maombi. Tunatumaini kwamba vidokezo vilivyo
elezwa humu zitakusaidia kuandaa CV bora kwa ajili ya mwajiri.
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv