Image result for LISHE KWA MTOTO
Lishe bora ni muhimu sana na wadau wengi wa afya ya watoto ikowemo shirika la chakula duniani (WHO) wanasisitiza na kuhamasisha wazazi kufikiria kuhusu maamuzi watakayofanya juu ya lishe ya watoto wao kama maamuzi ya afya. Msingi wa afya bora huchangiwa na lishe bora kwanzia mimba.
 Related image
Kwanza Kabla ya mimba mama anatakiwa ajiandae kwaaji ya kubeba ujauzito, kwa mfano mwanamke ambaye atabeba mimba akiwa na upungufu wa asidi ya foliki anaweza kupata mtoto mwenye mgongo wazi. Vyakula vyenye aside ya folik kwa wingi ni mboga za majani za kijani, matunda kama machungwa, maharage, nafaka zisizo kobolewa nk.

Na Mama mjamzito anatakiwa azingatie misingi ya lishe bora ili aweze kujipatia virutubisho vya kutosha kwa ajili yake na ya mtoto aliyeko tumboni mwake. Lishe bora huzingatia mchanganyiko wa vyakula mbalimbali, kiasi sahihi, ukamilifu wa virutubisho na kwa wakati sahihi. Lakini pia kuna ongezeko la uhitaji wa virutubisho vifuatavyo mfano protein, madini ya chuma, kalsiam na asidi ya folik.

Hivyo vyakula (nyama, samaki, mayai, vyakula vya jamii ya maharage, kokwa na mbegu mbegu, mboga za majani za kijani, maziwa na bidhaa zake, matunda na mboga mboga kwa ujumla) vyenye virutubisho twajwa hapo juu vinatakiwa viliwe kwa wingi ili kuhakikisha afya ya mama na mtoto atakaye zaliwa.

Lishe kwa watoto wa 0 mpaka miezi 6
Katika kipindi hiki cha miezi sita ya kwanza inashauriwa mtoto atumie maziwa ya mama tu bila kuchanga na kitu chochote hata maji. Maziwa ya mama yana virutubisho vyote anavyohitaji mtoto mchanga katika uwiano sahihi, hivyo hufanya maziwa ya mama yawe ni chakula bora na sahihi kwa mtoto mchanga kuliko maziwa mengine yoyote.  Hata kama mama anakwenda kazini, ni vizuri akikamua maziwa na kumwachia mwanae. Maziwa yakiwekwa kwenye joto la kawaida (room temperature) yanaweza kukaa masaa manne mpaka sita, yakiwekwa kwa jokofu hukaa mpaka siku tatu, yakikaa katika freezer hukaa kati ya miezi sita mpaka mwaka inategemee ubaridi wa freezer lenyewe.
 Related image
Faida za maziwa ya mama
Maziwa ya mama yana kinga mwili hasa yale maziwa ya mwanzo, humkinga mtoto na maambukizi na magonjwa mabilimbali, husaidia ukuaji muafaka wa ubongo hivyo mtoto kuwa na upeo mkubwa.

Maziwa ya mama ni safi na salama kwa mtoto wakati wote , na hupatikana kwa urahisi na hayana gharama, Lakini pia  yana joto sawia na joto la tumbo la mtoto hivyo hayawezi kudhuru utumbo wa mtoto.
Maziwa ya mama huzuia tatizo la kukosa choo kwa watoto, Unyonyeshaji unasaidia pia kuongeza mapenzi kati ya mama na mtoto.
Mama anayenyonyesha vizuri anaweza kujikinga na magonjwa mfano saratani ya matiti na kizazi na Mama anayenyonyesha vizuri anaweza kurudi  katika uzito wake wa kabla ya ujauzito

Uzalishaji wa maziwa
Wanawake huweza kutoa maziwa baada ya kujifungua chini ya ushawishi wa homoni za prolaktini na okistosini. maziwa ya kwanza kutolewa hujulikana kama kolostramu, ambayo huwa na kiwango cha juu cha imunoglobuliniIgA ambayo huzingira njia ya utumbo. Hii husaidia kulinda mtoto mchanga mpaka mfumo wa kinga yake unafanya kazi vizuri, na inajenga athari ya kupumzika, huondoa mekoniamu (choo cheusi cha kwanza cha mtoto) na kusaidia kuzuia kujengwa upya kwa bilirubini (sababu muhimu ambayo huchanjia ugonjwa wa macho kugeuka manjano).

Kuna sababu nyingi kwa nini mama hawezi kutoa maziwa ya kutosha. Baadhi ya sababu  ni kama ifuatavyo
Maswala ya kuridhi (katika familia hawana uwezo mkubwa wa kuzalisha maziwa) asilimia ndogo ya  wamama wenye shida hii.

Kushindwa kumuunganisha mtoto vizuri kwenye titi, Kutokujiandaa kisaikolojia kwaajili ya kumnyonyesha mtoto wako.

Ukosefu wa chakula au kupungukiwa na maji mwilini, Kutonyonyesha mara kwa mara
Maumivu, ugonjwa au matumizi ya dawa fulani zikiwemo dawa za uzazi wa mpango
Sonona na msongo wa mawazo

Jinsi ya kuongeza uzalishaji wa maziwa ya mama
Maandalizi ya kisaikolojia juu ya kunyonyesha mtoto wako kabla ya kujifungua
Kula chakula cha kutosha na hasa vimiminika mfano supu, juisi halisi na chai mfano chai ya mchaichai, chai ya mlonge, soya nk. ispokuwa (green tea, chai ya rangi na kahawa) hazishauriwi

Nyonyesha mara nyingi iwezekanavyo au kamua maranyingi uwezavyo
Muweke mtoto vizuri kwenye nyonyo ili kuongeza uzalishaji wa maziwa na pia kupunguza uwezekano wa kuumiza chuchu
Kutumia viungo mbalimbali katika vyakula vyako mfano, pilpili manga, mdalasini, hiliki nk.

Jaribu kuepuka msongo wa mawazo unaoepukika au tafutia suluhu msongo wa mawazo na sonona zitakazo jitokeza baada ya kujifungua.

Dalili zinazoonyesha mtoto anashiba vizuri
Mtoto ananyonya maziwa ya mama mara 6 mpaka nane kwa siku
Mtoto anapata choo kidogo zaidi ya mara 6
Wakati wa kunyonya unakuwa wa amani na furaha
Maziwa yanaisha kwenye nyonyo
Unaweza kumsikia mtoto akimeza mafundo ya maziwa
Mtoto anaongezeka uzito
Related image
Ushauri

Ni vizuri Mtoto aendelee kunyonya maziwa ya mama mpaka umri wa miaka 2. Baada ya miezi 6 ya kwanza mtoto huanza kula chakula cha nyongeza mfano uji nk. Kutokana na sababu mbalimbali mama akashindwa kumnyonyesha mtoto wake anaweza kumpatia maziwa maalumu kwa watoto (infant formula). Kama familia inauwezo wa kifedha mtoto aendelee kutumia maziwa maalumu ya watoto na si ya ng‘ombe mpaka atakapo timiza umri wa mwaka mmoja.

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top