Related image
Furaha ya kweli inatoka ndani yako. Haitoki nje, kwenye vitu, mali au chochote. Kwa lugha nyepesi ni kwamba sisi ndio tunaoweza kuamua kuwa na furaha au kuikataa. Ukiendelea kusubiri furaha kutoka kwenye vitu au hitimisho la lengo fulani ni wazi utakuwa unajidanganya, kwa sababu kuna mambo mawili, kukamilisha au kupata ulichokipanga au kushindwa. Kama utakipata ni wazi utakuwa na furaha, kama utakikosa utakosa furaha. Sasa kwanini uruhusu kukosa furaha pale unapokosa kitu?

Furaha ni hisia za raha au kuridhika. Hisia hizi hutoka ndani ya mtu. Mara nyingi kwa kutokujua watu huwa na fura wakati wanapoona mambo yao yameenda kama walivyoyatarajia. Yasipoenda kama walivyotarajia hukosa furaha kabisa. Kwa hiyo  jifunze kuwa na furaha katika maisha yako.
 Image result for Jinsi kujenga hisia za furaha
Haya hapa ni baadhi tu ya mambo yatakayo kusaidia kujenga hisia za furaha maisahani mwako ili kufika malengo yako:-

 Kwanza ; Kuwa na mtazamo chanya. 
Usipende kuangalia matatizo, vikwazo au mapungufu kwanza, penda kutafuta uzuri na ubora wa kitu kabla ya yote. Hii itakusaidia kuwa na mtizamo chanya.

Mtizamo utakaokuepusha na hisia hasi ambazo ni chanzo cha kukosa furaha. Kwa kufanya hivi utajenga mtizamo wa kusaidia jambo/kitu au mtu kuwa bora zaidi kuliko  kuona matatizo.

Pili ;Angalia matatizo kama daraja la kukuvusha hatua bora zaidi. 
Yaangalie matatizo kama daraja kwa sababu matatizo hukusaidia kukupima ulivyo imara na ukiyatatua yanakuongezea ujasiri zaidi. Kadhalika matatizo unayokutana nayo ni kengele inayokutaka kujifunza kitu katika safari yako ya maisha, na hivyo chukua hatua kwa kujifunza suala husika.

Mfano, ukiandamwa na madeni mengi, chukulia kuandamwa huko na madeni kama kengele inayokutaka ukae chini na ujifunze kuhusu fedha. Kwa mtizamo huu furaha itadumu ndani yako na utajenga imani kubwa ya kufanikiwa.

Tatu; Kuwa na imani ya kufikia kilele cha ndoto yako
Ukiwa na imani ya kufikia malengo au ndoto zako ni wazi utakuwa na furaha kila wakati. Maana chochote kitakachokuvuruga utakipuuza mara tu baada ya kufikiria mafanikio ya ndoto yako unayoyatekeleza. Ukiweza kuunganisha imani ya kufika ndoto yako na hisia zako ni wazi utakuwa na furaha kila mara.

Nne; Kuwa mwenye tija. 
Kuwa mwenye faida kwa jamii yako. Fanya shughuli zako kwa bidii kubwa na uongeze thamani kwa wengine. Wafanye watu kutegemea huduma bora kutoka kwako. Kwa kufanya hivyo utakuwa umejihakikishia furaha ya kudumu.


Tano; Thamani mahusiano yako na wengine. 
Jali sana mahusiano yako ya ndoa, ndugu zako, marafiki zako, wafanyakazi wenzako, jamaa zako na jamii kwa ujumla. Usimpuuze mtu yeyote wathamini wote, hii itakuchochoa kuwa furaha kila mara. Wote hao watakusamini na kukupenda hivyo furaha itakuja kama tunda la thamini unayowapa.

Sita; Jenga afya yako ya kiroho.
Ili ni eneo muhimu sana katika hali ya kuwa na furaha na kufanikiwa. Ukiwa vizuri kiroho utakuwa vizuri pia kihisia kwa sababu hakuna furaha ya ajabu kama kuwa karibu na Muumba yaani Mungu Mwenyezi, yeye ambaye ni asili ya uwepo wetu. Kila roho ina kiu na Mungu.

Saba; Tenga muda wa kushirikiana na kujumuika pamoja. 
Kujumuika na wenzako ni jambo muhimu katika kutunza na kuzalisa hisia za furaha. 


Nane na mwisho; Timiza wajibu wako. 
Ukitimiza wajibu wako, iwe ni kazini, nyumbani au katika jamii unakuwa mwepesi na inakupunguzia mawazo ambayo mara nyingi huondoa hisia za furaha ndani yako.

Usikubali kuhahirisha mambo fanya mara moja yakamilike ili uwe mwepesi kuanza majukumu mengine ukiwa huna kiporo cha majukumu. Kwa kufanya hivyo kila mara utajikuta mtu mwenye furaha na akili iliyotulia, kitu ambacho ni chema sana katika kukufikisha kwenye mafanikio.
Image result for Jinsi kujenga hisia za furaha

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top