Lishe bora ni muhimu sana na wadau wengi wa afya
ya watoto ikowemo shirika la chakula duniani (WHO) wanasisitiza na kuhamasisha wazazi kufikiria
kuhusu maamuzi watakayofanya juu ya lishe ya watoto wao kama maamuzi ya afya.
Msingi wa afya bora huchangiwa na lishe bora kwanzia mimba.
Kwanza Kabla ya mimba mama anatakiwa ajiandae kwaaji ya kubeba ujauzito,
kwa mfano mwanamke ambaye atabeba mimba akiwa na upungufu wa asidi ya foliki
anaweza kupata mtoto mwenye mgongo wazi. Vyakula vyenye aside ya folik kwa
wingi ni mboga za majani za kijani, matunda kama machungwa, maharage, nafaka
zisizo kobolewa nk.
Na Mama mjamzito anatakiwa azingatie misingi ya
lishe bora ili aweze kujipatia virutubisho vya kutosha kwa ajili yake na ya
mtoto aliyeko tumboni mwake. Lishe bora huzingatia mchanganyiko wa vyakula mbalimbali,
kiasi sahihi, ukamilifu wa virutubisho na
kwa wakati sahihi. Lakini pia kuna ongezeko la uhitaji wa virutubisho
vifuatavyo mfano protein, madini ya chuma,
kalsiam na asidi ya folik.
Hivyo vyakula (nyama, samaki, mayai, vyakula vya jamii ya maharage, kokwa na
mbegu mbegu, mboga za majani za kijani, maziwa na bidhaa zake, matunda na mboga
mboga kwa ujumla) vyenye virutubisho
twajwa hapo juu vinatakiwa viliwe kwa wingi ili kuhakikisha afya ya mama na
mtoto atakaye zaliwa.
Lishe kwa watoto wa 0 mpaka miezi 6
Katika kipindi hiki cha miezi sita ya kwanza inashauriwa
mtoto atumie maziwa ya mama tu bila kuchanga na kitu chochote hata maji. Maziwa
ya mama yana virutubisho vyote anavyohitaji mtoto mchanga katika uwiano sahihi,
hivyo hufanya maziwa ya mama yawe ni chakula bora na sahihi kwa mtoto mchanga
kuliko maziwa mengine yoyote. Hata kama mama anakwenda kazini, ni vizuri
akikamua maziwa na kumwachia mwanae. Maziwa yakiwekwa kwenye joto la kawaida
(room temperature) yanaweza kukaa masaa manne mpaka sita, yakiwekwa kwa jokofu
hukaa mpaka siku tatu, yakikaa katika freezer hukaa kati ya miezi sita mpaka
mwaka inategemee ubaridi wa freezer lenyewe.
Faida za maziwa ya mama
Maziwa ya mama yana kinga mwili hasa yale maziwa
ya mwanzo, humkinga mtoto na maambukizi na magonjwa
mabilimbali, husaidia ukuaji muafaka wa ubongo hivyo mtoto
kuwa na upeo mkubwa.
Maziwa ya mama ni safi na salama kwa mtoto
wakati wote , na hupatikana kwa urahisi na hayana gharama, Lakini pia yana joto sawia
na joto la tumbo la mtoto hivyo hayawezi kudhuru utumbo wa mtoto.
Maziwa ya mama huzuia tatizo la kukosa choo kwa
watoto, Unyonyeshaji unasaidia pia kuongeza mapenzi kati
ya mama na mtoto.
Mama anayenyonyesha vizuri anaweza kujikinga na
magonjwa mfano saratani ya matiti na kizazi na Mama anayenyonyesha
vizuri anaweza kurudi katika uzito wake wa kabla ya ujauzito
Uzalishaji wa maziwa
Wanawake huweza kutoa maziwa baada ya kujifungua
chini ya ushawishi wa homoni za prolaktini na okistosini. maziwa ya kwanza
kutolewa hujulikana kama kolostramu, ambayo huwa na kiwango cha juu cha
imunoglobuliniIgA ambayo huzingira njia ya utumbo. Hii husaidia kulinda mtoto
mchanga mpaka mfumo wa kinga yake unafanya kazi vizuri, na inajenga athari ya
kupumzika, huondoa mekoniamu (choo cheusi cha kwanza cha mtoto) na kusaidia
kuzuia kujengwa upya kwa bilirubini (sababu muhimu ambayo huchanjia ugonjwa wa
macho kugeuka manjano).
Kuna
sababu nyingi kwa nini mama hawezi kutoa maziwa ya kutosha. Baadhi ya sababu
ni kama ifuatavyo
Maswala ya kuridhi (katika familia hawana uwezo
mkubwa wa kuzalisha maziwa) asilimia ndogo ya wamama wenye shida hii.
Kushindwa
kumuunganisha mtoto vizuri kwenye titi, Kutokujiandaa kisaikolojia kwaajili ya kumnyonyesha
mtoto wako.
Ukosefu
wa chakula au kupungukiwa na maji mwilini, Kutonyonyesha mara kwa mara
Maumivu,
ugonjwa au matumizi ya dawa fulani zikiwemo dawa za uzazi wa mpango
Sonona
na msongo wa mawazo
Jinsi
ya kuongeza uzalishaji wa maziwa ya mama
Maandalizi
ya kisaikolojia juu ya kunyonyesha mtoto wako kabla ya kujifungua
Kula
chakula cha kutosha na hasa vimiminika mfano supu, juisi halisi na chai mfano
chai ya mchaichai, chai ya mlonge, soya nk. ispokuwa (green tea, chai ya rangi
na kahawa) hazishauriwi
Nyonyesha
mara nyingi iwezekanavyo au kamua maranyingi uwezavyo
Muweke
mtoto vizuri kwenye nyonyo ili kuongeza uzalishaji wa maziwa na pia kupunguza
uwezekano wa kuumiza chuchu
Kutumia
viungo mbalimbali katika vyakula vyako mfano, pilpili manga, mdalasini, hiliki
nk.
Jaribu
kuepuka msongo wa mawazo unaoepukika au tafutia suluhu msongo wa mawazo na
sonona zitakazo jitokeza baada ya kujifungua.
Dalili
zinazoonyesha mtoto anashiba vizuri
Mtoto
ananyonya maziwa ya mama mara 6 mpaka nane kwa siku
Mtoto anapata choo kidogo zaidi ya mara 6
Wakati wa kunyonya unakuwa wa amani na furaha
Maziwa yanaisha kwenye nyonyo
Unaweza kumsikia mtoto akimeza mafundo ya maziwa
Mtoto anaongezeka uzito
Ushauri
Ni vizuri Mtoto aendelee kunyonya maziwa ya mama
mpaka umri wa miaka 2. Baada ya miezi 6 ya kwanza mtoto huanza kula chakula cha
nyongeza mfano uji nk. Kutokana na sababu mbalimbali mama akashindwa
kumnyonyesha mtoto wake anaweza kumpatia maziwa maalumu kwa watoto (infant formula). Kama familia inauwezo wa kifedha mtoto
aendelee kutumia maziwa maalumu ya watoto na si ya ng‘ombe mpaka atakapo timiza
umri wa mwaka mmoja.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv