Furaha ya kweli inatoka ndani
yako. Haitoki nje, kwenye vitu, mali au chochote. Kwa lugha nyepesi ni kwamba
sisi ndio tunaoweza kuamua kuwa na furaha au kuikataa. Ukiendelea kusubiri
furaha kutoka kwenye vitu au hitimisho la lengo fulani ni wazi utakuwa unajidanganya,
kwa sababu kuna mambo mawili, kukamilisha au kupata ulichokipanga au kushindwa.
Kama utakipata ni wazi utakuwa na furaha, kama utakikosa utakosa furaha. Sasa
kwanini uruhusu kukosa furaha pale unapokosa kitu?
Furaha ni hisia za raha au
kuridhika. Hisia hizi hutoka ndani ya mtu. Mara nyingi kwa kutokujua watu huwa
na fura wakati wanapoona mambo yao yameenda kama walivyoyatarajia. Yasipoenda
kama walivyotarajia hukosa furaha kabisa. Kwa hiyo jifunze kuwa na furaha katika maisha yako.
Haya
hapa ni baadhi tu ya mambo yatakayo kusaidia kujenga hisia za furaha maisahani
mwako ili kufika malengo yako:-
Kwanza ; Kuwa na mtazamo chanya.
Usipende kuangalia matatizo,
vikwazo au mapungufu kwanza, penda kutafuta uzuri na ubora wa kitu kabla ya
yote. Hii itakusaidia kuwa na mtizamo chanya.
Mtizamo utakaokuepusha na hisia
hasi ambazo ni chanzo cha kukosa furaha. Kwa kufanya hivi utajenga mtizamo wa
kusaidia jambo/kitu au mtu kuwa bora zaidi kuliko kuona matatizo.
Pili ;Angalia matatizo kama daraja la
kukuvusha hatua bora zaidi.
Yaangalie matatizo kama daraja
kwa sababu matatizo hukusaidia kukupima ulivyo imara na ukiyatatua
yanakuongezea ujasiri zaidi. Kadhalika matatizo unayokutana nayo ni kengele
inayokutaka kujifunza kitu katika safari yako ya maisha, na hivyo chukua hatua
kwa kujifunza suala husika.
Mfano, ukiandamwa na madeni
mengi, chukulia kuandamwa huko na madeni kama kengele inayokutaka ukae chini na
ujifunze kuhusu fedha. Kwa mtizamo huu furaha itadumu ndani yako na utajenga
imani kubwa ya kufanikiwa.
Tatu; Kuwa na imani ya kufikia kilele cha
ndoto yako.
Ukiwa na imani ya kufikia malengo
au ndoto zako ni wazi utakuwa na furaha kila wakati. Maana chochote
kitakachokuvuruga utakipuuza mara tu baada ya kufikiria mafanikio ya ndoto yako
unayoyatekeleza. Ukiweza kuunganisha imani ya kufika ndoto yako na hisia zako
ni wazi utakuwa na furaha kila mara.
Nne; Kuwa mwenye tija.
Kuwa mwenye faida kwa jamii yako.
Fanya shughuli zako kwa bidii kubwa na uongeze thamani kwa wengine. Wafanye
watu kutegemea huduma bora kutoka kwako. Kwa kufanya hivyo utakuwa umejihakikishia
furaha ya kudumu.
Tano; Thamani mahusiano yako na
wengine.
Jali sana mahusiano yako ya ndoa,
ndugu zako, marafiki zako, wafanyakazi wenzako, jamaa zako na jamii kwa ujumla.
Usimpuuze mtu yeyote wathamini wote, hii itakuchochoa kuwa furaha kila mara.
Wote hao watakusamini na kukupenda hivyo furaha itakuja kama tunda la thamini
unayowapa.
Sita; Jenga afya yako ya kiroho.
Ili ni eneo muhimu sana katika
hali ya kuwa na furaha na kufanikiwa. Ukiwa vizuri kiroho utakuwa vizuri pia
kihisia kwa sababu hakuna furaha ya ajabu kama kuwa karibu na Muumba yaani
Mungu Mwenyezi, yeye ambaye ni asili ya uwepo wetu. Kila roho ina kiu na Mungu.
Saba; Tenga muda wa kushirikiana na
kujumuika pamoja.
Kujumuika na wenzako ni jambo
muhimu katika kutunza na kuzalisa hisia za furaha.
Nane na mwisho; Timiza wajibu wako.
Ukitimiza wajibu wako, iwe ni
kazini, nyumbani au katika jamii unakuwa mwepesi na inakupunguzia mawazo ambayo
mara nyingi huondoa hisia za furaha ndani yako.
Usikubali kuhahirisha mambo fanya
mara moja yakamilike ili uwe mwepesi kuanza majukumu mengine ukiwa huna kiporo
cha majukumu. Kwa kufanya hivyo kila mara utajikuta mtu mwenye furaha na akili
iliyotulia, kitu ambacho ni chema sana katika kukufikisha kwenye mafanikio.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv