Siri kubwa ya ushindi katika
maisha ni nidhamu katika kila kitu, unahitaji kuwa na nidhamu ya muda, pesa na
nidhamu katika malengo yako. Huwezi kufanikiwa kama utakuwa ni mtu wa hovyo
hovyo usiyejali. Lazima ujenge nidhamu ya hali ya juu. Leo unaweza kukuta watu
wengi wana ndoto kubwa sana maishani lakini ukijaribu kuangalia mienendo yao ya
maisha utaona ni kwa jinsi gani haiashirii hata kidogo kufika watakako.
Yafuatayo ni mambo ya muhimu ya kuyafanya ili kuilinda
siku yako na kuifanya kuwa na hamasa kubwa ya kuwajibika.
Anza siku kwa
kumshukuru Mungu.
Unaponia kupata mafanikio ni
lazima uwe na tabia ya tofauti kabisa na watu wengine. Jifunze kuwa na mazoea
ya kuanza siku yako kwa kumshukuru Mungu. Mungu ndiye akupaye fursa ya kuianza
siku nyingine hivyo una kila sababu ya kumshukuru. Na ukizingatia Mungu yu
nyuma ya mafanikio yako ni vyema pia kujikabidhisha kwa Mungu kabla ya
chochote.
jinenee mazuri.
Hili ni jambo ambalo wengi
hawalifahamu lakini linanguvu sana. Kujinenea mema ni moja ya njia ya kuufanya
ubongo kutoa nguvu kubwa ya ndani iliyojificha kukusaidia kutatua changamoto
zilizo mbele yako. Kadri unavyojinenea mazuri ndivyo kadri unafungua hamasa
kubwa ya kukufikisha utakako.
Epuka kusikiliza habari asubuhi.
Unapoamka asubuhi ubongo uko
tayari kupokea agenda itakayoongoza mwelekeo wa fikra na mawazo yako. Ukianza
na habari hasa za kwenye redio na televisheni hatari yake ni kwamba habari
nyingi katika midia zetu huwa ni habari hasi. Habari nyingi utasikia sijua
maafa sehemu fulani au migogoro kule nakadhalika. Hivyo kuanza siku na habari
utaelekeza fikra na mawazo yako kwa siku nzima kuwa na mwelekeo hasi tu.
Epuka kabisa mabishano. Mara
nyingi asubuhi hutumika na watu wengi kubadilishana mawazo hasa ya yale ambayo
usiku wote watu waliyasikia au kuyaona kwenye televisheni. Katika muda huu
ndipo mijadala na mabishano huzuka. Sasa kama unataka kuilinda siku yako epuka
kujihusisha na stori hizo ambazo hupelekea mabishano. Mabishano haya huwa ni ya
michezo, siasa, au ujuaji wa mambo.
Amka mapema sana. Ili
njia zote hizo hapo juu zifanikiwe ni lazima uanze kujenga mazoea ya kuamka
asubuhi sana, amka alfajiri kabla ya wengine. Hii itakusaidia kufanya mambo
yako kwa ufanisi zaidi kuliko kufukuzana na muda.
Ni jambo jema kuanza siku yako
ukiwa na hamu kubwa ya kupambana na kukamilisha ndoto zako. Hamasa ni nyezo
muhimu ya kukufanya kudumu katika kutenda kuelekea utakako. Weka katika matendo
yote tuliyoyajadili hapo juu.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv