Tatizo kubwa linalozuia watu wengi
kudhibiti matumizi ya kipato ni tabia yao ya kufanya matumizi ya kujionyesha
kwa watu, au kuigiza maisha ambayo hawana uwezo nayo. Hili linaendelea
kuwagharimu watu wengi sana, kama utaendelea kuishi maisha hayo kuwa na hakika
utaendelea kuona kipato hakitoshi, na zaidi utaendelea kujikita katika madeni
yasiona na umuhimu.
Tofauti iliyopo kati ya maskini
na tajiri, ni namna wanavyofanya matumizi ya fedha zao. Maskini yeye hutumia
kila fedha anayoipata lakini tajiri yeye hutumia kiasi cha fedha na kiasi
huhifadhi kama akiba, na akiba hiyo, huwasaidia kuwekeza ili kutengeneza fedha nyingine
zaidi.
Hebu
leo tuangalie njia ambazo unaweza kuzitumia ili kudhibiti matumizi ya hovyo ya
fedha:-
Jifunze kutumia bajeti kuongoza
matumizi yako.
Bajeti huwa ni muongozo wa
matumizi yako katika kipindi fulani cha muda. Usipokuwa na bajeti, utakuwa kama
mtu ambaye anabahatisha katika matumizi yake, maana chochote kitakachoonekana
mbele yake lazima kitamvutia na kukinunua. Utafiti unaonyesha kuwa aslimia
zaidi ya 50, ya matumizi ya fedha za watu wa kawaida, huelekezwa katika
matumizi ya vitu visivyo na umuhimu.
Tembea na fedha kidogo.
Jitahidi sna kujenga tabia ya
kutembea na fedha kidogo, au fedha za kile unachokwenda kununua tu. Acha fedha
nyingine nyumbani au jifunze kuweka fedha eneo ambalo si rahisi kulifikia kwa
haraka. Hii itakusaidia kutokufanya yale matumizi ya shinikizo.
Jipe muda kidogo kabla ya kununua kitu.
Unapojipa muda zaidi wa siku hata moja kabla kufanya
manunuzi ya kile ulichotaka kununua itakusaidia kujitathimini kweli kama
ulichokihitaji kukinunua kina umuhimu wowote kwako. Kwa sababu watu wengine
wawapo na fedha huwa hawatulii wanatamani tu kufanya matumizi.
Nunua kwa fedha taslimu.
Jitahidi kujiwekea falsafa ya
kununua kwa fedha taslimu tu, na kama huna fedha taslimu hutonunua chochote.
Siku hizi biashara nyingi zina ushindani mkubwa sana, na baadhi ya
wafanyabiashara hukopesha bidhaa zao kwa kipindi cha mienzi miwili, ili
kukuvutia wewe.
Hivyo unaweza kujikuta umeingia katika mtego wao, kukuvutia
ukope; na usipokuwa makini utajikuta unalimbikiza madeni lukuki. Kumbuka madeni
ni kikwazo kikubwa kuelekea kwenye uhuru wa kifedha.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv