Utafiti unaonesha baadhi ya vijana wengi katika kizazi cha sasa haswa wale wa kiume hawajui kabisa namna ya kufunga tai! na pindi inapotokea kuhitaji kuvaa tai.
Wengi wao hulazimika kuwaomba Wazazi, Walezi wao au baadhi ya watu
wanaojihusisha na mavazi kuwasaidia kufungia tai zao ili waweze kuivaa jambo ambalo kwa baadhi ya wafanyabiashara wa mavazi huwatoza gharama kwaajili ya kufanikisha zoezi hilo.
HISTORIA YA TAI
Kulingana na vyanzo mbalimbali, watu
walitumia mavazi fulani kabla tai hazijaanza kutumiwa katika Uingereza na
Ufaransa mwishoni mwa karne ya 16. Wanaume walivalia jaketi lililoitwa jaketi
la kubana. Walivalia kitambaa cha shingoni ili kujirembesha. Katika visa vingi
kitambaa cha shingoni, ambacho kingeweza kuwa na unene wa sentimeta kadhaa,
kilikuwa utepe wenye umbo la kisahani uliozingira shingo. Kilishonwa kwa
kitambaa cheupe na kufanywa kiwe kigumu ili kidumishe umbo lake.
Hatimaye, kola
inayoning’inia ikaanza kutumiwa badala ya kitambaa cha shingoni. Hii ilikuwa
kola nyeupe iliyofunika bega zima na ilining’inia juu ya mkono. Kola hizo
ziliitwa pia Vandykes. Miongoni mwa
wengine, zilivaliwa na Wapiuriti.
Katika karne ya 17, koti refu la ndani lililoitwa kizibao lilivaliwa
ndani ya koti refu la kawaida. Mwenye kulivaa alifunika shingo yake kwa
vitambaa vilivyoshabihi shali, au skafu. Kitambaa hiki kilizungushwa kwenye
shingo zaidi ya mara moja. Ncha zake zilining’inia mbele ya shati. Michoro ya
mwishoni mwa karne ya 17 huonyesha kwamba skafu zilipendwa sana wakati huo.
Skafu zilishonwa kwa kitambaa cha pamba, bafta, na hata gidamu. Zile
zilizoshonwa kwa gidamu zilikuwa ghali. Yasemekana James wa Pili wa Uingereza
alilipa pauni 36 na shilingi 10 kwa ajili ya skafu moja siku ya kutawazwa
kwake, bei ghali mno nyakati hizo. Skafu nyingine za gidamu zilikuwa kubwa.
Kinyago cha Charles wa Pili katika Makao ya Watawa ya Westminster chaonyesha
skafu yake ilikuwa na upana wa sentimeta 15 na urefu wa sentimeta 86.
Mafundo ya aina
nyingi yalitumiwa kufunga skafu hizo. Katika visa fulani utepe wa hariri
uliwekwa juu ya skafu ili kuishikilia kisha ikafungwa katika fundo kubwa chini
ya kidevu. Mtindo huu wa tai uliitwa solitaire. Fundo hilo
lilishabihi bow tie ya kisasa. Yasemekana
kwamba kulikuwa na angalau njia mia moja za kufunga skafu. Yasemekana kwamba
Mwingereza Beau Brummell, aliyechangia sana mitindo ya mavazi ya wanaume,
alitumia asubuhi nzima kufunga skafu moja ili kuhakikisha iko sawa kabisa.
Kufikia miaka ya
1860, skafu yenye ncha ndefu ilianza kushabihi tai za mtindo wa kisasa na
ikaitwa tai. Pia iliitwa tai yenye fundo la kitanzi. Jina hilo lilitokana na
fundo lililotumiwa na madereva wa gari lililokokotwa na farasi wanne. Shati
zenye kola zikawa ndio mtindo. Tai ilifungwa chini ya kidevu, na ncha zake
ndefu zilining’inia mbele ya shati. Wakati huo ndipo tai za kisasa zilipotokea.
Aina nyingine ya tai, bow tie, ilianza kupendwa
katika miaka ya 1890.
Watu fulani waweza kuwa na maoni hususa kuelekea mtu wasiyemjua
ikitegemea aina ya tai anayovalia. Hivyo, ni jambo la hekima kuvalia tai safi
zenye vigezo au rangi zinazofaana na shati, suruali, au jaketi lako.
Wapaswa kufunga fundo unalochagua kwa njia nadhifu. Labda fundo la
kitanzi ndilo linalopendwa sana. (Ona mchoro kwenye ukurasa wa 14.)
Ni nadhifu na la kiasi nalo hukubaliwa
katika sehemu nyingi kunapokuwa na sherehe rasmi. Fundo jingine linalopendwa ni
fundo pana isivyo kawaida, ambalo ni kubwa kwa kadiri fulani. Kwa kawaida
kibonyeo kidogo hufanyizwa kwenye tai chini tu ya fundo.
Wanaume wengi hawapendi kufunga tai. Hawapendi kusongwa kwenye shingo
zao. Hata hivyo, wengi ambao wamepatwa na tatizo hilo wamegundua kwamba saizi
ya shati ndiyo humkosesha mtu starehe. Ikiwa una tatizo hilo, hakikisha kwamba
kola ya shati yako si ndogo sana. Inapokuwa ya saizi inayofaa, huenda hata
usitambue kwamba umefunga tai.
Katika nchi nyingi tai huonwa kuwa sehemu muhimu ya mavazi rasmi au ya
kazi. Kwa sababu hiyo wanaume wengi Wakristo huvalia tai wanapojihusisha na
sehemu mbalimbali zilizo rasmi za huduma yao. Naam, tai yaweza kumwongezea
mwanamume adhama na kumfanya aheshimike.
Jinsi ya kufunga tai kwa fundo la kitanzi
1 Anza na ncha ya tai iliyo pana karibu sentimeta 30 chini
ya ncha nyembamba, na kuizungusha kwenye upande mwembamba, ukiirudisha upande
wa chini.
2 Izungushe tena ncha pana, na kuipitisha kwenye pindo.
3 Ukiwa umeshikilia sehemu ya mbele ya fundo bila kuikaza
kwa kidole cha shahada, vuta upande mpana ndani ya pindo kuelekea mbele.
4 Kaza fundo polepole, ukishikilia upande mwembamba na
kutelezesha fundo kwenye kola.
fuata video hii kujua kiundani zaidi..........
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv