Haiba ni nini? Watu wengine watafikiria
tunazungumzia mwonekano wa mtu kimavazi. Lakini haiba ni neno pana zaidi ya
mwonekano wa mtu kwa nje. Haiba ni jumla ya tabia za mtu zinazotokana na kile
anachofikiri, anachopenda, anavyojichukulia yeye mwenyewe, anavyowachukulia
watu wengine na kadhalika.
Haya yote hujenga mwonekano
wa mtu unaopimika (tabia) kama vile anavyoongea na watu, anavyodhibiti hasira
zake, anavyofanya maamuzi, anavyoweza kuwa mwaminifu, anavyoweza kutunza siri
moyoni, anavyoweza kukabiliana na changamoto, anavyovaa na mambo kama hayo
mengi mengi mengi.
Haiba hii tunayoizungumzia hujengwa na mambo mengi. Tunaweza kutaja kurithi kama sehemu muhimu ya utengenezaji wa haiba. Hapa tunazungumzia kemikali zinazoongoza mienendo ya mwili ama homoni (kwa kutohoa). Ujue wingi ama uchache wa homoni fulani huchangia kujengeka kwa tabia fulani. Pia mazingira alimokulia mtu, kwa maana ya watu na malezi aliyopata na kadhalika.
Ni vyema kujua kuwa haiba ya mtu hubadilika kuendana na umri. Kila umri unazo changamoto zake zinazoathiri haiba ya mtu husika.

Na tunajua kuwa kila mtu hurithi kitu tofauti kutoka kwa wazazi wake. Maana hata ndugu wa damu wnaatofautiana uthirishwaji huu wa kibaolojia. Mazingira yanayomzunguka mtu nayo ndiyo usiseme. Tunatofautiana kupindukia. Ni kwa sababu hiyo tunaweza kusema kuwa haiba hutofautiana kati ya mtu na mtu.
Haiba ziko nyingi - tutaziangalia mbeleni - lakini ninachotaka kusema hapa ni kwamba tusithubutu kufanya majumuisho kwa kuwaweka watu katika makundi fulani ya jumla jumla ya kinadharia. Kwa mfano kusema kuwa wanawake wote wanatabia fulani, ama wanaume wote wanatabia fulani ni makosa ya kiufundi.
Sababu si kila mwanamke ana haiba inayofanana na mwanamke mwingine. Na pia haiba ya mwanamke huweza kubadilishwa kutokana na haiba ya mume aliyenaye. Yaani kama mwanamke huyo angeolewa na mwanamme mwenye haiba nyingine, mwanamke huyo huyo angekuwa na haiba nyingine kabisa.
Tabia ya mwanamke wa ndoa fulani inatokana na jinsi haiba yake iliyoingiliana na ile ya mume wake. Mke huyo japo anaonekana kuwa na haiba isiyoridhisha katika ndoa B angeweza kuwa na haiba njema zaidi laiti kama angekuwa na ndoa C na mume mwingine kabisa.
KUmbe kabla hujaamua kuishi na mtu, wapaswa kupima hata suala la haiba zetu wawili! Umuhimu wa haiba ndugu msomaji.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv