Related image
Uvaaji wa vikuku ni urembo pia ni utamaduni wa mwafrika, Awali urembo huu ulionekana zaidi katika baadhi ya makabila ya kiafrika ukivaliwa na watu wa rika zote; kuanzia watoto wachanga, wasichana, wanawake wa makamo, hata wazee.

Kwa baadhi ya makabila hayo, vikuku vimekuwa vikivaliwa kama mila kwamba kila mwanamke anapozaliwa lazima avae urembo huo kwa kufuata desturi na tamaduni zao, tofauti na ilivyo sasa ambapo wengi huvaa kama urembo wa kawaida.

Vikuku hivyo vyaweza kuwa vya shanga, ngozi au hata madini kama dhahabu, fedha na shaba. Kikuu kinaweza kuvaliwa mguu mmoja au miguu yote.

Wanajaamii wengi wamekuwa na mtazamo tofauti kuhusu uvaaji wa vikuku wakihusisha na mambo yasiyofaa na kuonyesha kuwa wengi wanaovaa urembo huo wamepotoka, au kwenda kinyume na maadili ya kitanzania.
Image result for maana ya vikuku
Kwa mujibu wa wadau wa urembo kikuku kinapaswa kilegee kidogo katika mguu na kwamba hakipendezi kikiwa kimebana, kwani licha ya kusababisha matatizo katika kuruhusu damu kutembea, hakiwezi kuwa na mwonekano mzuri kikiwa katika hali hiyo.

Bila shaka katika mitindo inayoonekana kupokelewa vizuri na wanawake hasa wasichana ni pamoja na uvaaji wa vikuku ambao sasa umetikisa katika kila nyanja.


Kwa hiyo Vikuku ni tamaduni za kiafrica. ni urembo wa kupendezesha kiungo kama kuvaa cheni shingoni, helen sikioni, pete kidoleni, bangili mkononi, kipini puani shanga kiunoni na kikuku mguuni.


tukiangalia hata kabila la wamasai, hadi wanaume nao wanavaa tena ni wote, sasa  tuacheni fikra potofu watanzania, lile ni pambo msilitafsiri kiviile. 
Related image
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top