Image result for rangi za nguo
Rangi  zinaweza kuelezea tabia ya mvaaji kwa harakaharaka hata kama haumfahamu kama moja ya chapisho la jarida la Readers Digest linavyoeleza.

Tukianza na rangi Nyeupe
Rangi hii hubeba nadharia ya usafi. Humfanya mvaaji aonekane mtu anayependa usafi si wa mwili tu bali hata tabia kwa neno zuri ni ‘purity’.Pia rangi hii husimama sehemu nyingi, haichagua sehemu ya kuvaa.

Nyeusi
Watu wengi hupendelea nguo nyeusi. Rangi hii humpa mvaaji mwonekano wa kujiamini na jasiri, ndiyo maana watu wengi hupendelea kuvaa mavazi yenye rangi nyeusi wanapokwenda kwenye usaili wa kazi.

Njano
Ni rangi ambayo mtu akivaa anaonekana mwenye furaha wakati wote. Hata kama mtu ana huzuni na masononeko moyoni, akivaa nguo ya rangi hii humwelezea kuwa ni mtu wa furaha na anayependa kuwa na furaha siku zote.

Nyekundu
Hii ni rangi inayoonyesha nguvu na kwamba una uwezo wa kufanya chochote.Ukivaa nguo nyekundu hata katika mkusanyiko wa watu wengi mtu anaweza kupita. Hata kama hujiamini hiyo rangi itakuaminisha na ndivyo watu watakavyokuchukulia.

Bluu
Hii inakuonyesha umetulia, watu huwa na mawazo chanya na mtu anayevaa nguo yenye rangi ya bluu. Mvaaji anaonekana siyo mtu wa kutetereka na kwamba ana uwezo wa kukabiliana na jambo lolote. Pia rangi ya bluu huvaliwa sana kwenye usaili wa kazi.

Kijani
Rangi ya asili, mara nyingi inahusishwa na mazingira.Ukivaa nguo ya rangi ya kijani unaonekana mtu anayejali, mtunzaji na mpenda mazingira. Mtu anayedumisha asili, watu wengi wanaofuga rasta ‘marasta’ hupenda kuvaa nguo zenye rangi za kijani.

Zambarau
Zambarau inamwongelea mvaaji kama ni mtu mbunifu na mtu anayependa sana kuvaa, hapitwi nyuma na mitindo ya kisasa.

Kahawia
Unapovaa nguo ya rangi hii unaonekana mtu uliyetulia na mtu anaweza kukuamini hata pasi kukufahamu. Mtu asiyependa makuu, mtu watu.

Related image
Imeandaliwa na Suzan Mwilo- mwananchi


 JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top