Related image
Tunapokuja katika suala la mahusiano  mazuri lazima Wewe kijana au mwanaume ujue kuna mambo mhimu ambayo uantakiwa kuwa nayo ili kumpata umpendae unatakiwa kujua  nini cha kufanya kwa ajili ya kulifanya penzi lako lizidi kuchanua na kuwa jipya kila kuchapo.

KUJIAMINI
Mwanamke anajisikia salama zaidi akiwa na mwanaume ambaye anajiamini – mwenye uwezo wa kutetea hoja zake na kujieleza sawia. Siyo anayebabaika. Wakati mwingine, mwanamke anaweza kukupima hata katika jambo ambalo amekosea yeye, ataangalia unavyotoa maamuzi yako na, atafuatilia kuona kama utakuwa mwepesi wa kuyabadilisha maamuzi yako.

KUJALI
Wanawake wanapenda sana wanaume wanaojali Kama huna tabia hiyo, ujue upo katika nafasi kubwa ya kumkwaza mpenzi wako. Mjali mpenzi wako kwa kila hali. taka kujua maendeleo yake,mpe  nafasi kubwa sana ya kuendelea kudumu katika uhusiano hai.

USAFI BINAFSI
 Asilimia kubwa ya wanawake wanapenda sana usafi. Mwanamke anavutiwa sana na mwanaume mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini kuwa na wewe.

KUJITETEA
Wakati unapodai haki yako mbele ya mwanamke wako, suala la kujitetea linapewa nafasi kubwa sana.
Wanawake hawapendi kuwa na wanaume ambao wapo tayari kuonewa. Wanataka wenye uwezo wa kusimama kidete kuona haki zao hazichukuliwi kirahisi.

UKARIBU
Hapa namaanisha  kuwa naye katika mambo mengi unayoyafanya kila siku. Ni vizuri kuwasiliana naye mchana, ukitaka kujua aina ya chakula alichokula siku hiyo au ikiwezekana mchagulie na mambo mengine kama hayo.

KUMSIFIA
Usipuuzie hili  Hali ni tofauti sana kwa wanawake ambao hupenda kuwasifia wanaume zao. Msifie mkpenzi wako tu kwa zile sifa alizo nazo usuzidishe na za uongo.

MALENGO
Image result for MALENGO
Wanaume wengi hawapendi kuwashirikisha wanawake katika mambo yao. Usifanye mabo yako kwa siri bila kumshirikisha mwenza wako mshirikishe katika malengo yako na kile unachofanya.

KIPAUMBELE
Mpe mpenzi wako kipaumbele katika mambo tofauti tofauti unayokuwa unafanya muonyeshe kuwa yeye n wa maana na mhimu katika maisha yako.

TENDO LA NDOA
Image result for TENDO LA NDOA

Hakika hili ni jambo  nyeti, kinachohitaji lugha nzuri ya kirafiki kukifafanua. Hakuna siri, tendo la ndoa ni moja ya kiwakilishi cha ndoa. Kimsingi tendo la ndoa lina nafasi yake. Ni muhimu likaheshimiwa na kutengewa muda maalum wa kufurahia. Acha papara kabisa.

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz ,twiter@edonetz ,inst@edonetz_blog na youtube@edone tv
 
Top