1. Hakikisha midomo yako sio mikavu kabla hujaanza kujipaka lipstick, kwa kupaka 'lip balm' au
mafuta kidogo ya mgando kwa ajili ya kuipa unyevunyevu.

2. Unaweza pia kutumia 'concealer' kidogo unayopaka usoni kupaka juu ya midomo yako, husaidia
kufanya lipstick idumu kwa muda mrefu mdomoni.

3.Jipake wanja unaoendana na rangi ya lipstick unayotaka kujipaka, husaidia kuifanya lipstick
ikae vizuri pamoja na kukupa muonekano mzuri mdomoni.

4.Paka lipstick yenye rangi uipendayo; ila hakikisha kama midomo yako ina asili ya kuwa mikavu,
usitumie lipstick kavu badala yake paka ambayo ina mafuta.

5.Baada ya kujipaka lipstick unaweza kujipaka 'lip gloss' kidogo, kwa ajili ya kung'arisha
muonekano wako japo siyo lazima sana.
 
Top