Tumbaku ( tumbako) ni majani (minoga) makavu ya mtumbaku ambayo yanatumiwa na binadamu kwa kuvuta kama sigara, kutafuniwa mdomoni au tumbaku ya kunusa. Tumbaku huwa ndani yake kemikali ya nikotini ambayo mwili unazoea haraka sana na kuifanya vigumu kwa wavuta tumbaku kuachana na desturi hii.

Asili ya tumbaku ni Amerika ambako Maindio wenyeji waliitumia kama dawa ya kidini pia ya burudani. Tangu Kolumbus Wahispania walipeleka mtumbaku hadi Ulaya ambako uliangaliwa mwanzoni kama mmea wa kiganga. Matumizi hasa kwa njia ya kuvuta na kutafuna yalienea haraka katika Ulaya na kwa njia ya mabaharia Wareno katika pande zote za dunia.

Kilimo cha tumbaku ni tawi muhimu la uchumi kwa nchi mbalimbali. Kilwa mavuno ya duniani ni takriban tani milioni 6.7. Wazalishaji wakuu ni China (39.6%), Uhindi (8.3%), Brazil (7.0%) na Marekani (4.6%). Tanzania ni kati ya nchi kumi za kwanza zinazolima tumbaku inavuna asilimia 1.6 ya tumbaku ya dunia.

Historia ya kilimo cha tumbaku nchini Tanzania inakwenda nyuma mwanzoni mwa miaka 1960. Ukiacha mkoa wa Songea unaolima tumbaku ya moshi (DFC), mikoa mingine iliyobaki inalima tumbaku ya mvuke (FCV). Mkoa wa Mara kwa kiasi kikubwa unalima tumbaku ya mvuke katika wilaya za Tarime, Serengeti na Rorya. Kuna kiasi kidogo cha tumbaku ya moshi kinachozalishwa katika maeneo yaliyotengwa. Mkoa wa Morogoro kwa sasa unazalisha tumbaku ya mvuke katika maeneo ya Kilosa (Kimamba, Msowero na Kidonga) na Ulanga. Kwa muhtasari tumbaku hulimwa hapa nchini katika maeneo kama inavyoonekana hapa chini;Tabora, Urambo, Sikonge, Kahama, Manyoni, Mpanda, Kigoma, Iringa, Chunya, Morogoro, Mara, Songea.

Mavuno hutokea siku 70 hadi 130 baada ya kulima shamba. Majani huvuniwa wakati majani yanaanza kuonyesha rangi ya manjano maana yameiva. Mavuno yanaenda kwa uangalifu kwa sababu mashimo katika majani yanapunguza ubora na bei, Baada ya mavuno majani yanafungwa pamoja kwa kamba na kukaushwa. Kuna mbinu za kuzikausha polepole kivulini au juu ya moto au penye hewa ya moto haraka katika muda wa siku chache tu.

Majani yaliyokauka hufungwa pamoja kwa mchakato wa kuchachua. Huu unabadilisha ladha ya tumbaku kwa njia inayotakiwa. Baadaye tumbaku hutiwa sosi zenye sukari au vitu vingine vya kutia ladha halafu kukatwa na kufungwa kulingana na matumizi kama tumbaku ya kuvuta katika sigara za kawaida, sigara kubwa, pipo, ya kutafunia au ya kunusu.

Utaratibu wa uzalishaji wa tumbaku nchini Tanzania

Uzalishaji wa tumbaku hufanyika kupitia kilimo cha mkataba. Kilimo cha mkataba kimefanywa katika sekta ya tumbaku kwa miaka mingi. Tumbaku nchini huzalishwa zaidi kwa utaratibu wa kimkataba kupitia kilimo cha mkataba kwa kushirikisha pande mbili yaani mnunuzi wa tumbaku na wakulima. Awali hii ilihusisha mnunuzi kusambaza pembejeo za kilimo ikifuatiwa na masoko ya tumbaku. Mnunuzi ananunua tumbaku kutoka kwa mkulima. Kama ilivyo sasa, mkataba unategemea hasa makubaliano kwa mnunuzi kununua tumbaku inayozalishwa (Mikataba ya ununuzi wa tumbaku mbichi).

Mageuzi ya sasa ya zao la tumbaku yameleta mabadiliko muhimu kwenye kilimo cha mkataba kama ilivyo desturi katika sekta ya tumbaku. Mipango ya kilimo cha mkataba ya awali iliwashirikisha wanunuzi na wakulima tu. Wadau wengine hawakuhusika. Kama sehemu ya mageuzi katika zao, kumekuwa na marekebisho katika sheria ya sekta ya tumbaku ili kupanua wigo na taratibu za kilimo cha mkataba katika sekta ya tumbaku ikiwa ni pamoja na kushirikisha taasisi za kifedha, wauzaji wa pembejeo, wawekezaji, wasindikaji na mtu yeyote mwenye nia ya kusaidia mkulima wa tumbaku kwa kuzingatia makubaliano.  inaendelea BOFYA HAPA 

 
Top