Taarifa zilizopo Tanzania kutoka FAO zinakadiria kwamba mahindi yanalimwa kiasi cha hekta milioni 4.12 za ardhi na kuzalisha tani milioni 5.36 za mahindi ya kula ambazo ni sawa na wastani wa tani 1.3 kwa hecta (FAOSTART, 2013). Kwa thamani, mahindi ni zao la nne kwa umuhimu kwa mazao ya kilimo yanayozalishwa hapa Tanzania baada ya nyama ya ng’ombe, ndizi na maharage makavu.
Katika kuzalishwa kwa wingi, mahindi ni zao la pili baada ya mihogo.
• Mahindi: ni zao muhimu katika usalama wa chakula (na mbegu)
• Matumizi kwa chakula: ni gramu 308 kwa mtu mmoja kwa siku moja. Mahindi yanachangia wanga asilimia 61, protini asilimia 50, na ni asilimia 75 ya nafaka zote.
• Wazalishaji wakuu: wakulima wadogo kwani huzalisha asilimia 85.
• Eneo: Mahindi ni asilimia 45 ya mazao yote yanayo zaa kwa msimummoja na ni asilimia 60 ya nafaka za Tanzania.
• Kiuchumi: mahindi yanachangia takriban asilimia 20 ya mapato yoteyatokanayo na kilimo katika taifa (GDP) (NAP-Sera ya kilimo ya Taifa,2013).
• Uzalishaji kwa kanda za ikolojia: Nyanda za juu kusini 46% ya mahindiyote - ~90% yanaenda kwenye ghala la Taifa, kanda ya ziwa (17%),Kanda ya Kaskazini + kanda ya kati (14%), kanda za Kusini, Mashariki naMagharibi (23%).
Mahindi yanastawi vizuri katika kanda zenye mvua ya wastani lakini kumekuwa na ongezeko la wakulima wadogo kulima zao hili maeneo yenye uzalishaji hafifu, maeneo yenye uhaba wa mvua na yenye uwezo hafifu wa uzalishaji. Hali hii ni tete na mkulima anaweza asivune hata kidogo kwenye maeneo hayo.
Hatari ya kupata mavuno kidogo au kukosa mavuno kabisa inaweza kurekebishwa kwa kutumia mikakati mbalimbali kama ifuatavyo:
• Wakulima katika maeneo makame wanaweza kushauriwa kupanda mazao yanayostahimili ukame kama mtama;
• Mahindi yanaweza kupandwa kwa ufanisi zaidi iwapo wakulima wata-fuata teknolojia na mbinu sahihi kama kilimo kwa kufanya matumizi bora na uhifadhi wa maji;
• Matumizi ya mbegu bora zinazokomaa mapema na zinazovumilia ukame;
• Kupanda kwa wakati;
• Kilimo hifadhi;
• Kufuatilia taarifa za utabiri wa hali ya hewa;
• Kupanda kwa nafasi sahihi;
• Njia sahihi za kuchanganya au kubadilishana mazao ya mahindi na mikunde kwa nafasi na nyakati tofauti;
• Matumizi ya mbolea za viwandani kwa kuzingatia S4 yaani zao sahihi, kiwango sahihi, kwa wakati sahihi, na kutumia njia sahihi pia matumizi ya mbolea za asili kama mabaki ya mazao na samadi;
• Palizi ya uhakika na yenye tija;Njia za kupunguza madhara ya wadudu waharibifu na magonjwa, pia kuzingatia S4. INAENDELEA BOFYA HAPA