Kahawa ilianzishwa kwanza Kilimanjaro na wamishonari Wakatoliki mwaka 1898. Aina ya Botanical imeongezeka

kiuchumi

Kahawa ni mojawapo ya mazao makuu ya biashara yanayosafirishwa nchi za nje, ikichangia kiasi cha 5% ya mapato ya jumla bidhaa zinazosafirishwanje, na inazalisha mapato ya wastani wa Dola za Marekeni millioni 100 kwa mwaka kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita. Tasnia hii hutoa mapato ya moja kwa moja kwa zaidi ya kaya za wakulima 450,000, hivyo, kusaidia utafutaji wa riziki wa watu wanaokadiriwa kuwa milioni 2.4. Wastani wa uzalishaji wa mwaka kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita umesimama kwenye kiwango cha tani 50,000 ambapo uzalishaji unaendelea kupungua na uwezekano wa ubora haukutumika / hauzingatiwi kikamilifu,hivyo kuchangia katika kupata bei ndogo za shambani na kuendeleza umaskini wa vijijin. Kwa kuzingatia fursa zilizopo kwenye soko la Kimataifa, na uwezekano wa kuzalisha kahawa ya ubora wahali ya juu, kwenye ngazi ya Kimataifa (ikijumuisha Arabika laini pamoja na Robusta) Tanzania ingekabiliana na matatizo machache sana katika uuzaji wa kiasi kikubwa cha kahawa kwa bei inayoleta faida sana ilimradi uzalishaji unaongezeka.

Mikahawa ya Arabia ya Tanzania hupandwa kwenye mteremko wa Mlima Kilimanjaro na Mlima Meru katika maeneo ya kaskazini, chini ya kivuli cha miti ya ndizi, eneo la nje la kahawa ya Afrika Mashariki, pia katika mikoa ya Kusini  Mbeya na Ruvuma ambako kahawa imefungwa na ndizi na maeneo mengine ni safi. Kahawa ya Arabia hufanya hadi 70% ya jumla ya uzalishaji wa nchi. Inaendelea .. BOFYA HAPA

 
Top