Kila mmoja wetu anaekuwa katika mahusiano hasa yale mahusioano
mazuri wengi upenda kujua hatima yao ila ushindwa kubaini na kutambua kama ni
mapenzi ya ndoa au ni ya muda tu, Mwanamke na mwanaume wanapokuwa kwenye kilele
cha mapenzi, ni rahisi sana kila mmoja kuchunga kauli zake na kuongea yale
ambayo yatamvutia mpenzi wake ili kila mmoja awe na mvuto kwa mwenzake na
hivyo kuwa karibu zaidi. Hata hivyo watu wengi (hususan wanawake)
wanashindwa kung’amua kwamba, katika mapenzi kila mmoja ana lake moyoni,
na ni vigumu kujua mwenzako anawaza nini juu yako.
Ni vyema kama mwanamke akiamua kujiingiza kwenye uhusiano, basi
awe na uhusiano na mwanaume ambaye anaonekana dhahiri kuwa ni muoaji na si
wa kumchezea tu, na kuingia mitini. Unaweza kujiuliza kuwa
utamjuaje mwanaume muoaji na yule ambaye si muoaji bali wa kukuchezea tu.
Leo tuyaangazie baadhi ya mambo muhimu yatakayomuwezesha
mwanamke kujua kama mwanaume aliye naye ni muoaji au anamchezea tu:
1. Katika mazungumzo yenu ya kawaida jaribu kuzungumzia kuhusu
maisha ya ndoa ili kuangalia kama yeye anayachukulia vipi.
Wanawake wengi hukwepa kuzungumzia maisha ya ndoa na
wapenzi wao kwa kuhofia kwamba wataonekana wanajipigia debe ili waolewe, lakini
hili ni jambo muhimu sana kulijadili.
Kwa nini?
Kwa nini?
Kwa sababu ni muhimu kwa wapenzi waliopendana na
kuaminiana kukaa na kujadili kuhusu matarajio ya kila mmoja ili kujua kama
wako kwenye mustakabali mmoja au la. Kwa kujadili kuhusu jambo hilo
kutawawezesha kujiwekea malengo ya namna ya kufikia matarajio yao.
Iwapo mwanaume ataonekana kutovutiwa na mazungumzo hayo,
basi hapo mwanamke ajue kwamba anachezewa na kama akiendelea na uhusiano
huo, basi ajue kwamba, amekubali kuchezewa.
2. Katu usijiaminishe kwamba kila mwanaume utakayekutana naye
na kukutongoza na kukuahidi kukuoa kuwa huenda akawa ndiye mtarajiwa,
Wanawake wengi wamekuwa na hamu kubwa ya kutaka kuolewa
na wanayatamani sana maisha ya ndoa. Wanaamini kwamba kila
mwanaume atakayemualika kuwa na mtoko naye hususan wa chakula cha mchana
au usiku ndiye mtarajiwa.
3. Ni vyema ukaangalia matendo yake zaidi kuliko maneno yake.
Hii ni muhimu sana. Mwanaume anaweza kukwambia kwamba wewe
ndiye chaguo lake atakayekuoa, na anaweza hata kukupeleka kwa Sonara au
duka la kuuza pete za uchumba za dhahabu na kukununulia pete ya uchumba ya
gharama, lakini kama hataanza kuchukua hatua muhimu za kukutambulisha kwao
kwa ajili ya kupata Baraka za wazazi wake au kujitambulisha kwenu
kwa ajili ya kupata Baraka za wazazi wako Basi ujue kwamba hayo ni
maneno matupu na katu hayavunji mfupa.
4. Kama mwanaume akiwa mkweli na kukueleza kwamba anakupenda
lakini hana mpango wa kuoa hivi karibuni,
usilazimishe kujenga uhusiano naye kwa nia ya kutaka
kumshawishi ili akuoe. Kama kuna mambo ambayo mnaendana na umevutiwa kuwa
naye karibu, si vibaya kujenga naye urafiki wa kawaida usiohusisha
mapenzi. Lakini ni vyema kuwa makini kwani wakati mwingine urafiki wa
kawaida na mwanaume unaweza kukufikisha mahali ambapo hukutarajia.
5. Tengeneza aina ya maisha yatakayokutambulisha jinsi ulivyo
na matarajio yako pamoja na msimamo wako kuhusu mahusiano.
Hiyo itakufanya kujenga uzingativu kwenye matarajio yako na
haitakuwa rahisi kwako kwenda kinyume na malengo uliyojiwekea hasa
pale atakapojitokeza mwanaume atakayetaka kujenga mahusiano na wewe.
Jiunge nasi kupitia
fb@edonetz,
twiter@edonetz, inst@edonetz_blog na youtube@edone tv