Kuna Utafiti
kuhusu wanaume wafupi unasema wanaume wafupi wana mapenzi ya kweli na ya
dhati kuliko wanaume warefu, kitu ambacho siwezi bisha sababu, wanawake wengi
huwa hawapendi kutoka na wanaume wafupi kwahiyo inawachukua sana muda kupata
mwenza na lazima wawapende na wawape mapenzi ya kweli wanawake zao ili wasiwaache
kwa sababu wanawake wengi wanapenda mwanaume warefu na wengi wana
mvuto kuliko wafupi.
Wanawake wengi wanapenda kutoka na wanaume ambao wamewazidi urefu hata
kidogo, kuliko kuwa na mwanaume ambaye ni mfupi kuliko wao,wengi wanasema hii
inaleta picha mbaya au muonekano mbaya wakiwa wanaongozana lakini kuna sifa
nyingine za wanaume wafupi wanawake wengi wanasema zinawakera kama,
Wivu
Inasemekana wanaume wafupi wana wivu wa kupindukia na sio kama wanaume
wengine warefu hawana wivu ila wivu wao unapitiliza kiasi cha kukera kwani wivu
ukizidi sana ni kero katika mapenzi.
Wanaume wengi wafupi wana sifa sana, kiasi cha kukera wanajisifia sana,
na wanataka sana kuonekana, kama wapo eneo Fulani wakiingia sehemu mtajua kama
kuna mtu kaingia sababu ya sifa zao na maneno yao japokuwa pia wana sifa moja
ya kuwa wachechi sana.
Gubu
Hapa sasa ukichanganya na wivu ni balaaa maana mwanaume mwenye gubu ni
zaidi ya mwanamke muongeaji, Gubu ni ile hali ya kukosoa kila kitu,kila kitu
kibaya, yeye haridhiki na chochote na hata utaonekana huwezi chochote
akiwa karibu, hilo gubu au hata kama kila kitu kipo sawa atatafuta sababu ya
kuongea tu.
Wanajidai
Wanajua kila kitu. ( Much know)
Much knows, hapa bwana unakutana na mtu kila kitu anajua yeye, ni
kero sababu akiwa mbele za watu atataka kila mtu ajue anajua nini kama
inaongelewa siasa, mpira au mapenzi yeye fundi wa kila kitu, kitu ambacho
kiukweli kinakera sana wakati mwingine.
Muonekano/
Mvuto
Wanawake wengi wasema wanaume wafupi hawana mvuto sana, kama wanaume warefu, kwahiyo hiyo ni moja ya sababu ya wao kutotaka kutoka na wanaume wafupi, japokuwa sio wanaume wote wafupi hawana mvuto. Japokuwa inasemekana siku hizi hakuna anae angalia urefu wako uzuri wako watu wanangalia sana mfuko wako tu, hayo ni maneno ya mitaani watu wanaongea. Mimi binafsi sijui kama ni hali halisi.
ungana nasi
fb@edonetz twiter@edonetz inst@edonetz na youtube@edonetz