nakuorodhoshea majengo 5 marefu kuliko yote duniani. Dubai ndiyo inabeba sifa ya kuwa na jengo lililopanda angani kuliko yote hapa duniani.
5.Shanghai World Financial Center: Shanghai, China

Shanghai World Financial Centre lina nafasi za ofisi, mahoteli na maduka kwenye ghorofa ya kwanza. Lina urefu wa futi 1,614 na ghorofa 101. Pia lina paa maalum la kuangalia mandhari lililoko juu zaidi duniani, futi 1,555 kutoka ardhi
4.Taipei 101: Taipei, Taiwan
Jengo la Tapei 101 linanyanyuka futi 1,669. Lina ghorofa tano za chini y ardhi na 101 kwenda angani. Ndilo jengo refu zaidi duniani lililojengwa kwa kuzingatia ubora wa mazingira.Wakati wa sherehe za kitaifa, fashi fashi huwashwa kwenye jengo hili.

3.One World Trade Center: New York, NY
Pia hujulikana kama Freedom Tower, jengo hili lina urefu wa futi 1,776 feet, na lina ghorofa 104, na kulifanya kuwa refu zaidi katika mataifa ya magharibi. Lilijengwa kufikia futi 1776 kama kumbu kumbu ya mwaka ambao Marekani ilipata uhuru wake
2.Makkah Royal Clock Tower Hotel: Mecca, Saudi Arabia
Jengo linaitwa The Makkah Royal Clock Tower Hotel, lilijengwa katika jitihada za kuubadilisha mji mtukufu wa Makkah kuwa wa kisasa zaidi. Lina sifa kadhaa – ndiyo hoteli ndefu zaidi duniani, mnara wa saa ulioko juu zaidi duniani, na pia saa kubwa zaidi duniani. Lina urefu wa futi 1,972 na ghorofa 120.
1.Burj Khalifa: Dubai, United Arab Emirates
Jina lake ni Burj Khalifa, awali likijulikana kama Burj Dubai, hili ndilo baba na mama wa majengo kwa urefu duniani. Lina urefu wa futi 2,723 na ghorofa 163. Kazi ya ujenzi ilichukua miaka mitano, na ilikamilika mwaka 2009 katikati ya Dubai.

ahsante sana mtu mkubwa kwa kufuatilia www.edonetz.blogspot.com unaweza kushea kadri uwezavyo na kucoment chochote


 
Top