moja ya majengo
machache marefu barani Afrika ni PSPF Towers na ndiyo jengo refu zaidi
lililokamilika Afrika Mashariki na Kati, likiwa na urefu wa mita 147.
Jengo hilo
lililozinduliwa na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, ujenzi wake ulitumia miaka
minne tangu mwaka 2011 hadi 2015 limegharimu shilingi bilioni 139.20 za
Tanzania lina maeneo ya ofisi na nyumba za makazi 88. Pia katika jengo hili
kuna sehemu ya mgahawa, mabenki, bwawa la kuogelea, Sehemu za kufanyia mazoezi,
maegesho ya magari na sehemu nyingine muhimu.
Kudumu kwa rekodi ya
urefu ya PSPF Towers lenye minara miwili na ukubwa wa mita za mraba 73,000,
kutategemea kukamilika kwa majengo mengine yanayochipua kwa kasi katika Afrika.
Mtu mkubwa kwa walioka bongo watakuwa wanalijua vizuri jingo hili. walio
wengi huwa tunachukulia vitu vya nyumbani kawaida kawaida na hatupendi kuvipa kipaumbele
hila Tanzania tuna mali nyingi za kujivunia kila siku nitakuwa nakuandalia hapa
ndani www.edonetz.blogspot.com
usitoke kando yangu..