Mnamo mwaka 1960 wapiga picha wa
kujitegemea huko Italy walijipatia umaarufu mkubwa kutokana na filamu moja
iliyokuwa mashuhuri duniani iliyoenda kwa jina la La Dolce Vita (“Maisha
Matamu” kwa Kitaliani) iliyotengenezwa na Producer Federico Fellini wa
huko huko Italy.
Hadhithi ya filamu hiyo ya La Dolce Vita inamhusu mwanahabari mchunguzi aliyeitwa Marcello (muigizaji akiwa Marcello Mastroianni) na mpiga picha wake aliyeitwa Paparazzo (muigizaji Walter Santesso). Ingawa bado kuna ubishi wa maana ya jina “Paparazzo”, lakini mfanano wake na jina la mbu mkubwa aitwaye Papataceo kwa lugha ya Kitaliani, ilileta maana kwa kulinganisha maneno ya producer Fellini mwenyewe kwenye taarifa aliyotoa wakati huo.Fellini alisema Jina Paparazzo kwake yeye ni kama mbu anayeruka huku na kule akitafuna watu walio kwenye starehe zao,
na kuachia mchoro wa aina ya mtu asiye
na mifupa (angalia picha hapo juu kulia) akiwa ameshika kamera ambayo flashi
yake inawaka, akimaanisha kwamba paparazzi, kama walivyo mbu, ni wadudu
wasumbufu.
Baada ya filamu ya La Dolce Vita kuzinduliwa huko Italy, neno
(Papaparazzi) likawa linafananishwa na wapiga picha za udaku
waliokuwa wakiwinda nyota mbalimbali wa filamu na watu maarufu na kuwaanika
magazetini. Hata hivyo, Fellini alisema yeye hakuwa anawaiga hao wapiga
picha za udaku, bali alidai yeye anachofanya ni kuyaingiza magazeti katika
filamu, wakati stori zake zilizohusu maisha ya kuponda raha wanayoishi nyota wa
filamu ziliuza sana magazeti ya udaku.
Hapana shaka kwamba kuingia kwa neno Paparazzi katika lugha ya Kiingereza kunatokana na hiyo filamu ya La Dolce Vita, pale ilipozinduliwa nchini Marekani huo mwaka 1961. Na lilikuwa ni jarida maarufu la Time Magazine lililowezesha jina hilo la Paparazzi kupata umaarufu na kuwaganda wapiga picha wa kujitegemea waliokuwa wakisaka habari za udaku za nyota wa filamu.
Makala ya jarida hilo iliyokuwa na kichwa cha habari cha “Paparazzi on the Prowl” (yaani paparazzi mawindoni), pamoja na picha ya wapiga picha kibao waliokuwa wamezuia gari la Binti Mfalme mmoja aliyekuwa ziarani Rome, ndiyo vilivyokoleza moto.
Makala hiyo ilikuwa inazungumzia jinsi kundi la wapiga picha wa kujitegemea walivyokuwa kama mbwa mwitu mawindoni, wakipita huku na kule kuwinda watu wenye majina makubwa katika jamii, kuwapiga picha wakiponda raha na kuwaanika kwenye magazeti ya udaku.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
FACEBOOK@EDONETZ ,TWITER@EDONETZ
INSTAGRAM@EDONETZ NA YOUTUBE@EDONETZ TV