Kujitambua ni uelewa wa mtu binafsi kungamua yeye ni nani na kutambua nini anapaswa kufanya, kwa nini na sababu ipi. Muda gani na katka muktadha upi.
Elimu hii ya kujitambua ni adimu mno! Kwani hujikita ndani ya nafsi ya mtu na kumfanya kuonekana mwenye busara na hekima katika uongeaji ,kimaamuzi na kimatendo pia bila kufanya hivyo kiunafiki.Pia wapo ambao hujitia ukiziwi,ububu na wengine kuwa waropokaji ili waonekane wenye elimu ya kujitambua kumbe hamna kabisa hata chembe ya kujitambua.

FAIDA KUU YA KUJITAMBUA.
1 Kila akifanyacho mtu anayejitambua hulenga kuchochea na kuleta maendeleo katika jamii husika.
2 Kuwa jasiri Au msimamo dhabiti kwa analoamini ni sahihi bila kuyumbishwa na mtu yoyote.
3 Kufikia malengo chanya.
4 Huwa kioo cha jamii (unakuwa barua isomwayo na kila mtu katika jamii).
5 Kutenda matendo mema (kutetea haki za wanyonge,kupinga ufisadi,n.k) katika jamii
6 
Kutambua nafasi aliyonayo na jamii humuheshimu bila kushinikizwa
7 Mtu huyu huwa sio tegemezi katika jamii..
8 Kuwa ni mtu asiyekuwa na makuu, huwa na matumizi mazuri ya rasliamali.mfano raslimali watu,ardhi,pesa n.k
9 Kuwa ni mtu wa watu.
10 
Kuwa mbunifu (Creative) husoma nyakati.
11 Kuwa anatoa suruhu na sio kulalamika au kulalamikiwa na yeye kuanza kulaumu na huwa hakati tamaa mpaka siku ya kufa n.k

MATOKEO ENDAPO HUTOJITAMBUA

-Hathari ni kinyume cha faida tajwa na mjumuisho wa hili
-Kutojitambua huzorotesha maendeleo kwani mlengwa hufanya mambo hovyo hovyo).Na hii hupelekea miigogoro kuongezeka katika jamii

MWISHO WA YOTE KWA LEO
Waweza  kushangaza watu wasiojitambua huwa hawataki msaada wa kuwatoa katika utumwa wa kutojitambua ndio maana huwa wakali wa kutokubaliana na mkakati wa anayetaka kuwasaidia, wengine wakibeza na kuweka mbele vyeo, elimu, umri, pesa, uzuri, umbo n.k  japo wengine hukimbilia kujitetea kuwa binadamu hajakamilika wakati hawako tayari kukamilishwa na wale wenye kujitambua.Hivyo ni vyema mtu akibahatika kujigundua kuwa ana dalili za kutojitambua yambidi kujitafakari na kuanza kuchukua taratibu taratibu ili arudi kwenye mstari au kuingia kwenye msitari na kujifunza hakuna mwisho.

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW

FACEBOOK@EDONETZ  ,TWITER@EDONETZ INSTAGRAM@EDONETZ_BLOG NA YOUTUBE@EDONE TV
 
Top