Kama ujawai kujiuliza, kujua zaidi au
kufuatilia juu ya hili basi fuatilia kwa kina hili uweze kujua kiundani yaani Kama
ni ajabu vile, jinsi umbo lako lilivyo limetokana na siku yako uliyozaliwa. Ili
kujua hii njia inakupasa kujumlisha tarehe, mwezi na mwaka uliozaliwa ili upate
tarakimu ya mwisho ya namba.
Jinsi ya kujua njia
hii, kwa mfano umezaliwa 12.05.1990, unatakiwa ufanye hivi: 1 + 2 + 0 + 5 + 1 +
9 + 9 + 0 = 27 = 2 + 7 = 9.
Hii ina maana kwamba hiyo tarakimu ya mwisho
ni tarakimu inayoelezea umbo la mwili wako ulivyo ambayo ni 9 katika mfano huu.
Fanya hesabu hii ili uweze kujua namba yako na umbo lako binafsi; ukipata kati
ya mojawapo ya namba hizi maana yake kama ifuatavyo:
Namba
1
Watu hawa wanakabiliwa sana na
kitambi kutokana na ukweli kwamba metabolism yao inafanya kazi kwa kiasi
kidogo sana na ipo chini sana.
Namba 2
Watu hawa wananyemelewa sana na
kitambi ila mara nyingi watu hawa wanapendelea kufanya diet. Hata hivyo
watu hawa wanakosea katika diet yao kwa kutojua chakula kipi hasa cha kula
wakishikwa na njaa. Tahadhari kwa watu hawa inawapasa kutumia sana matunda,
mboga za majani na mazoezi ya miili yao.
Namba
3
Watu hawa wana mtazamo wa kupenda sana mambo
ya dunia na hii inachangia mzigo wa kiroho kuwaandama na kubadilisha uzito wao
kwa ujumla.
Namba
4
Watu hawa wanashauriwa kujihusisha sana na
mazoezi ya miili yao, kwa sababu ukosefu wa mazoezi kwa miili yao
itawasababishia njaa na tamaa, ambayo kwa upande mwingine itasababisha
mkusanyiko wa mafuta mwilini.
Namba
5
Watu hawa wanajua unene utayaharibu maumbo
yao. Watu hawa wapo na maumbo madogo kiasi, wanapenda kuyafurahia maisha kwa
kuzuia mkusanyiko wa mafuta katika miili yao.
Namba
6
Watu hawa wanachukuliwa kama watu wa bahati,
wenye maumbo sawia, wanakula kwa kiasi na kwa kuyatunza vizuri maumbo yao.
Namba
7
Watu hawa kwa kawaida wanaongezeka uzito
kutokana na masuala ya hisia, ambapo wakiweza kuwa na mahusiano mazuri na ya
kudumu na wapenzi wao itawasaidia katika maisha yao.
Namba
8
Watu wa kundi hili wanashauriwa kujifunza
kuacha mambo mengine yapite na kusamehe, kama wakiwa na hasira za mara kwa mara
itachochea kuongeza mkusanyiko wa mafuta na kuongezeka kwa uzito.
Namba
9
Hatimaye, watu hawa wanakabiliwa na tishio la
kitambi na ongezeko la mafuta. Kupunguza uzito kwa watu hawa mara nyingi
inakuwa vigumu. Kuzuia ongezeko la mafuta kwa watu hawa ni jambo la muhimu na
inawapasa watumie matunda yenye tindikali.