usilolijua ni kama
usuku wa giza na wakati wewe ukisema cha nini mwenzio analia atakipata lini
hili linajidhihilisha juu ya utando wa buibui tuuchukuliao kama uchafu katika
maeneo yetu lakini ukweli uko hivi…
Utafiti
mpya ulioripotiwa na Gazeti la Nano Letters la Marekani unaonesha kuwa utando
wa buibui ni malighafi nzuri ya kimaumbile ya kutengeneza darubini, na inaweza
kutumiwa kuinua uwezo wa darubini za jadi za kuangalia vitu vidogovidogo
viilivyotengenezwa kwa vioo. Kama bado ulikuwa hujaipata hiyo sasa ufahamu na
kutilia maanani utafiti ulioongozwa na Dk. Wang Zengbo kutoka Chuo Kikuu cha
Bangor cha Uingereza kwa kushirikiana na Prof. Fritz Vollrath kutoka Chuo Kikuu
cha Oxford.
Kutengeneza
darubini kwa utando wa buibui ni rahisi sana. Watafiti waliweka utando wa
buibui juu ya kitu kitakachoangaliwa, kutia kileo katika kitu hicho na
utando wa buibui, halafu kuangalia kitu hiki kupitia darubini ya kawaida ya
vioo. Utando wa buibui unainua uwezo wa darubini ya vioo kwa mara mbili hadi
tatu, na kuwawezesha kuona vitu vidogovidogo vyenye urefu wa nanomita 100 tu.
Wakitumia darubini ya vioo tu hawawezi kuona.
Dk. Wang
amesema aligundua jambo hili kwa bahati. Siku moja alipocheza na mtoto wake
katika ua wa nyumba yake aliona utando wa buibui. Ghafla akapata wazo la
kutengeneza darubini kwa utando huo, baadaye alithibitisha kuwa wazo hili kweli
linafanya kazi.
JIUNGE NASI
FACEBOOK@EDONETZ, TWITER@EDONETZ INST@EDONETZ_BLOG NA YOUTUBE@EDONE TV