kuna mambo mwanaume unaweza kuyachukulia kimzaa mzaa hila hakika
penzi litakua na kukua kila iitwapo leo endapo utazingatia suala hili kwa
ukaribu na kiundani zaidi unatakiwa kulijua na kuliweka katika ratiba zako za
kila siku
iko hivi Mwanasaikolojia na Mwalimu kutoka Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam maarufu kama Chriss Mauki ambaye ameongelea swala la
mawasiliano kuwa moja ya vitu ambavyo wanawake wanapenda ingawa wanaume wengi
wanashindwa kutekeleza hilo swala kwa kuona halina umuhimu. Yaani wanawake wanapenda mawasiliano wanapenda uwasiliane
wajue uko wapi unafanya nini na nani, wanaume wengi wakishaulizwa maswali kama
haya wanakuwa wakali, kuna mahitaji ambayo wote wanafanana na kuna vile
wanavyovipenda kama kuambiwa ukweli lakini mwingine anakataa mimi bora
asiniambie kitu chochote.
Wanawake wanapenda ukaribu kujali
hisia zake, kuzungumza nae kuonesha una mjali, kuonesha unamuamini na kumpa
kipaumbele katika maisha ya kawaida hata kwenye mahusiano, vile vile mwanamke
anapenda kujaliwa katika matatizo na kusifiwa pale anapofanya kitu sahihi
hii pia ni katika maisha ya mapenzi na hata nje ya mapenzi. Katika mahusiano
mwanamke anapenda kuhakikishiwa ulinzi na usalama wake kiafya, kihisia na
kiuchumi pia mazungumzo ni muhimu kwa sababu mwanamke huumizwa sana na vipindi
virefu vya ukimya sio tu kwamba wanataka mazungumzo bali mazungumzo yenye
kuleta hamasa katika maisha na yenye mvuto ndani yake.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
FACEBOOK@EDONETZ ,TWITER@EDONETZ
INSTAGRAM@EDONETZ NA YOUTUBE@EDONETZ TV