huenda kila siku wewe mama au dada unajiuliza ni kitu gani
unaweza kumfanyia mwenza wako hili azidi kukupenda lakini badoinakuwa vigumu
kuelewa, na mkikutana faragha unaonyesha ufundi na ujuzi wa hali ya juu lakini
bado unaona penzi linalega lega na halisimami kama matarajio yako yalivyo.
Sasa Katika kukomesha tatizo kama hilo, jua vitu unavyodhani ni
vidogo kumbe ndio tatizo kubwa kabisa katika mausiano hayo sasa mwanamke
anatakiwa kujiepusha na kufanya mambo yafuatayo kwa kadiri iwezekanavyo na
kutoyakaribia maeneo haya nyeti ambayo huwakera wanaume wengi:
1 .KUTOKUWA
NA SIRI ZA MATATIZO BINAFSI:
Unaweza ukawa unazungumza na
marafiki zako kuhusu baadhi ya mambo yaliyofanywa na mumeo, lakini kufichua
baadhi ya siri ambazo mumeo amekupatia kwa kukuamini ni jambo hatari sana, na
unatakiwa kutojaribu kufanya hivyo kwa sababu ya unyeti wake; mwanaume anapenda
mkewe awe hazina ya siri zake na mshauri wake katika mambo yake yote. Hivyo,
jitahidi sana kuficha na kutunza siri za mumeo, usizitangaze.
2. KUTOMJALI MAMA YAKE: Mama anaendelea
kuwa mwanamke namba 1 katika maisha ya wanaume wengi, hivyo kutolikaribia eneo
hili itayafanya maisha yako kuwa maridhawa.
3. KUNG’ANG’ANIA MABADILIKO YA MWENZA:
Wanaume wengi wanaamini kuwa wanawake hufanya kazi ya kuwabadilisha wenza wao
kuwa kama wanyama wanaofugwa kwa kuwasukuma wafanye kazi na mambo wasiyoyapenda
au wasiyoyataka kabisa. Hili ni eneo nyeti sana katika ndoa hasa pale mke
anapomlinganisha mume na watu wengine. Iwapo unataka kumuelekeza mumeo kufanya
jambo fulani usimlinganishe na watu wengine, mshauri kwa njia nyingine.
Kuamiliana naye kwa namna hii kunamfanya ahisi kuwa unampa changamoto.
4. MALEZI BORA YA WATOTO:
Wakati fulani
wanandoa huzozana kwa sababu ya suala la malezi ya watoto. Mke anaweza kuhisi
kuwa mume anamlea mtoto na kumfundisha baadhi ya mambo kwa njia isiyofaa.
Usimkataze tu kumlea mtoto kwa njia anayeoitaka, lakini zungumza naye vizuri
kuhusu mambo anayotakiwa kumfundisha na yale ambayo mtoto hatakiwi kujifunza
kwa umri wake.
5 . KUMUACHIA UPWEKE MDA MWINGI:
Kutoka pamoja na marafiki zako kwa muda mrefu na kumuacha mumeo nyumbani kwa
kipindi kirefu inaweza kumkera mumeo. Vivyo hivyo, iwapo hutamtilia manani
mumeo na badala yake ukawa ni mtu wa kuangalia televisheni peke yako, inamfanya
mume ahisi kuwa ni mtu aliyetelekezwa na asiyepewa umuhimu.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
FACEBOOK@EDONETZ ,TWITER@EDONETZ
INSTAGRAM@EDONETZ NA YOUTUBE@EDONETZ TV