Africa?
Bado kuna mabishano ya ni nini hasa asili ya jina Africa. Wengine wanadai linatokana na neno la Kigiriki la APHRIKE, lililomaanisha kusikokuwa na baridi, ama la Kilatini APRICA, lenye kumaanisha nchi yenye jua daima.
 Wengine wanasema neno "Afrika" limetokana na lugha ya Kilatini ya Waroma wa Kale. Waroma kwa jina hilo hawakumaanisha bara lote bali eneo katika jimbo la Carthage ama Tunisia ya leo tu. Asili yake ni kabila la "Afrig" lililoishi sehemu zile.
Wakati huo Wagiriki wa Kale walitumia zaidi jina la Libya kwa ajili ya nchi kusini ya Bahari ya Mediteraneo. Maeneo ya ndani kuelekea kusini mara nyingi yaliitwa kwa jina la "Ethiopia" linalomaanisha nchi ya watu weusiweusi (kwa Kigiriki "aithiops": aliyechomwa na jua).
Katika ramani za kale kutoka Ulaya maneno yote matatu ya "Afrika", "Lybia" na "Ethiopia" yanapatikana yakitumika kama jina la bara. Jina la "Afrika" limekuwa kawaida kuanzia karne ya 16 BK.

Misri ya wakati huo ilikuwa inachukuliwa kama sehemu ya bara la Asia,na alikuwa Mwanajiografia aitwaye Ptolemy (85-165A AD) ambaye aliigawa Afrika na Asia na Ulaya kwa kuchora ramani inayoonesha Suez na Bahari Nyekundu kuwa ndio mpaka baina ya Asia na Afrika.
 
Top