Mtoto wa kwanza aliyetengezwa kwa
kutumia mbinu ya uzazi wa mbegu za watu watatu amezaliwa, jarida la kisayansi
la New Scientist limetangaza.
Dkt John Zhang akiwa na mtoto huyo |
Iko hivi Mtoto huyo wa kiume
mwenye umri wa miezi mitano ana chembe chembe za DNA kutoka kwa mamake, babake
pamoja na jeni za mfadhili.
Madaktari wa Marekani walichukua hatua hiyo kuhakikisha kuwa
mtoto huyo wa kiume atakuwa huru kutokana na hali ya jeni ambayo mamake kutoka
Jordan anabeba katika jeni zake.
Wataalam wanasema kuwa hatua hiyo ni mwamko mpya wa kimatibabu na inaweza
kusaidia familia nyingine zilizo na hali za jeni zisizokuwa za kawaida.
Lakini wameonya kuwa uchunguzi wa mara kwa mara wa mbinu hiyo
mpya ya kiteknolojia inayoitwa ufadhili wa Mitochondrial unahitajika.
Mitochondria ni vyumba vidogo vidogo ndani ya kila seli ambavyo
hubadili chakula kuwa nguvu inayotumika mwilini.
Baadhi ya wanawake hubeba jeni zilizo na kasoro na wanaweza
kupitisha jeni hizo hadi kwa watoto wao.
Wanasayansi waliohusika katika shughuli hiyo walisafiri hadi
Mexico kwa sababu huko hakuna sheria za kuzuia shughuli kama hiyo ya
kimatibabu.
Walichukua sehemu muhimu za chembe za kinasaba (DNA) kutoka kwa
yai la mama, na DNA ya mitochondria kutoka kwa yai la mfadhili na kuunda yai
lenye afya ambalo lilitungshwa mbegu kutoka kwa baba.
Matokeo yake ni kuzaliwa kwa mtoto mwenye 0.1% ya DNA kutoka kwa
mfadhili na jeni nyingine zote, zinazoamua sifa kaa vile rangi ya nywele na
macho kutoka kwa mama na baba.
Dkt John Zhang, mkurugenzi wa kimatibabu katika hospitali ya New
Hope Fertility Centre jijini New York City, anasema yeye na wenzake walitumia
njia hiyo kupata viinitete vitano, lakini wakastawisha kimoja tu.