Umewahi kusikia
vimbunga vikiwa na majina ya kushangaza, mfano cha sasa kinachoitwa Matthew
ambayo kimekumba maeneo ya Haiti, Jamaica, Jamhuri ya Dominika, Bahamas na
baadhi ya majimbo ya Marekani.
Muda kidogo
uliopita kulikuwa na kimbunga kingine kilichojulikana kama Hermine ambacho
kilisababisha uharibifu mkubwa jimbo la Florida.Lakini
kinachokumbukwa sana ni
kile kwa jina Katrina ambacho kiliathiri sana majimbo ya Louisiana, Mississippi
na Alabama nchini Marekani.
Je, vimbunga hivi hupewa vipi
majina? Ni hivi..
Vimbunga vinavyopewa majina
Vimbunga
katika maeneo ya bahari ya Atlantiki, maeneo ya Caribbean na Ghuba ya Mexico
hupewa majina ya Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) ambalo lina
makao yake makuu nchini Uswizi.
Zamani,
ni majina ya kike pekee yaliyotumiwa lakini kuanzia 1979, majina ya kiume
yalianza kutumiwa.
Huwa
kuna makundi sita ya majina ambayo hutumiwa kwa mzunguko.
Hii
ina maana kwamba majina yaliyotumiwa kwenye vimbunga mwaka hu hayatatumiwa tena
hadi 2022.
Majina
kwenye orodha hii yanaweza kubadilishwa na WMO.
Orodha
hii ilianza kutumiwa mwaka 1979. Kabla ya hapo, jina la kimbunga Fern
lilibadilishwa mwaka 1966 na badala yake kukatumiwa Frieda. Hakuna sababu
iliyotolewa.
Majina yanavyoacha kutumiwa
Baadhi
ya majina huacha kutumiwa, sana kunapotokea uharibifu mkubwa au hasara kubwa
hivi kwamba kutumia tena jina hilo kutafufua kumbukumbu zenye uchungu.
Mfano
ni kimbunga Katrina kilichoua watu 2,000 mwaka 2005 na kusababisha uharibifu
mkubwa Marekani.
Kimbunga
hicho kiliwaacha watu milioni moja bila makao. Mji wa New Orleans, Louisiana
uliathirika sana.
Katika
WMO kuna kundi la wataalamu liitwalo Kamati ya Vimbunga vya Tropiki ambalo
hukutana kila mwaka.
Kundi
hilo ndilo huamua ni majina yapi yatatumika tena na ni yapi yataacha kutumiwa.
Majina yaliyoacha kutumiwa
Kando
na Katrina, kuna majina mengine ambayo yameacha kutumiwa. Mitch, kutokana na
kimbunga cha mwaka 1998 kilichoua watu 11,000 Honduras na Nicaragua, halitumiwi
tena. Kimbunga hicho ndicho kibaya zaidi kukumba maeneo ya Magharibi mwa dunia
katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.
Kimbunga
Sandy cha mwaka 2012 na Kimbunga Irene 2011 pia vilisababisha uharibifu mkubwa.
Majina hayo hayatumiwi tena.
Kimbunga
hatari zaidi kuwahi kukumba Marekani kilitokea 1780, ambapo kiliua watu 22,000
maeneo yaMartinique, Barbados na St Eustatius.
Wakati
huo majina hayakuwa yameanza kutumiwa kurejelea vimbunga.
HURRICANE
CENTER
Majina maeneo mengine duniani
Katika
maeneo mengine duniani, huwa kuna utaratibu tofauti wa kuvipa majina vimbunga.
Lakini
majina yote hupitia kwa WMO.
Kwa
mfano, maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa Pasifiki na Bahari ya China Kusini,
kuna jedwali la majina ambalo kila taifa linaloathirika huchangia.
Baada
ya kimbunga kutokea, kimbunga kinachofuata hupewa jina linalofuata.
Kwa
mfano, kimbunga cha kwanza huitwa Damrey (kimbunga cha kwanza Cambondia) na
kitakachofuata kinafaa kuitwa Kaikui (jina la kwanza China).
Kimbunga
cha sasa maeneo hayo ni Chaba (jina la nafasi ya nne Thailand).
Kilichotokea
majuzi kiliitwa Megi na ambacho kiliathiri maeneo ya China na Taiwan. Jina hilo
ni la nafasi ya nne chini ya majina ya Korea Kusini
METEOROLOGICAL ORGANISATION
Majina
ya vimbunga na tufani yalianza kutumiwa Uingereza na Ireland, kwa majaribio.
Kuna
jina kwa kila alfabeti, isipokuwa Q, U, X, Y na Z, ambao ndio utaratibu
unaotumiwa kuvipa majina vimbunga Atlantiki Kaskazini.
Source Bbc