Hakuna kitu kinacholeta mkangamyiko katika ndoa kama migogoro ya
mawifi yaani ndugu wa mume hadi wengine utakuta wanarushiana maneno makali bila
sababu za msingi ingawa sio wote hila walio wengi wako vile na Maisha ya ndoa
ni matamu sana ikiwa mume na mke wataishi kwa amani na upendo, kubwa hao mawifi
hujiona wana haki zaidi kuliko mwanamke huyo kwa sababu mumewe ni ndugu
yao wa damu, lisikupe shida hili fanya yafuatayo.
TUMIA BUSARA KATIKA MAAMUZI
Lazima uwe na busara na moyo wa uvumilivu ili uweze kukabiliana na mawifi
wakorofi. Mwingine anaweza akawa analala kutwa nzima bila kusaidia kazi za
nyumbani halafu mume anapokuja jioni anakuwa wa kwanza kumwambia maneno ya
ajabu, Hata kama amemwambia kaka yake kuwa labda hushindi nyumbani, baada
ya yeye kuondoka asubuhi na maneno mengine mengi kutokana na chuki zake
binafsi, unapaswa kutumia busara za hali ya juu. tumia lugha nzuri ni wazi kuwa
mumeo atakuelewa na kukusamehe ambapo naamini kuwa usiku huo utakuwa wenye kila
aina ya furaha na bashasha zilizojaa cheche za mapenzi.
MTAMBUE TOKEA MWANZO ALIKUWAJE?
Jinsi unavyoanza ndivyo unavyomaliza, kama ukivurunda kitu
kuanzia mwanzo, tarajia kuharibu mpaka mwisho. Kinachotokea mwishoni ni
kupunguza madhara ya tatizo ambalo tayari limeshatokea na lina madhara
makubwa, Inawezekana tangu ulipokwenda kijijini kwao (ukweni) ulishaona
baadhi ya tabia zake mbaya ambazo kwa namna moja ama nyingine zilikukwaza.
Kwanza mumeo atakapokupa taarifa ya ujio wa wifi yako, usioneshe
kukasirika, kwa sababu kama ukionesha umekasirika, anaweza akahisi jambo fulani
baya kwako, Pengine atahisi humpendi dada yake hivyo hata siku akikukosea
na kumwambia ataamini ni fitina au chuki zako binafsi. Siku wifi yako anapokuja
nyumbani, kuwa wa kwanza kumkumbusha mumeo kwenda kumpokea kituoni, weka
maandalizi motomoto na onyesha furaha ya ujio wake.
MALIZENI WENYEWE KWA MAZUNGUMZO
Ikiwa wifi yako amekukosea jaribu kuzungumza naye. Inawezekana
ghafla alianza kuwa na maneno ya hapa na pale au wivu usioeleweka, pengine
alimwambia mumeo, kuwa una tabia mbaya au vyovyote katika kukuharibia ndoa
yako. Usionyeshe chuki, zungumza naye taratibu, Mueleze jinsi unavyompenda
na kuuthamini uhusiano wenu. Ikiwa utatumia lugha nzuri naamini atakuelewa
lakini kama siyo muelewa ataendelea na chokochoko zitakazokukera.
MSHIRIKISHE MUMEO
Kama yote hapo juu hayakufua dafu, unapaswa kukaa chini na mumeo
na kumweleza juu ya jambo hili. Kukaa kwako kimya na kumvumilia kutakuwa hakuna
maana, kwa sababu ni rahisi ndoa yako kuvunjika, Usimfiche chochote, hata
kama aliwahi kukutolea maneno machafu kwa mumeo, usijali, zungumza taratibu
bila jazba huku ukitumia hoja kuliko maneno matupu!!!!!
Nyumba ni kwa ajili yako na mumeo. Kuolewa hakumaanishi kwamba
umeolewa na ukoo mzima na kila mmoja anaweza kukudhihaki na
kukutukana, Lazima utambue haki yako na kama mumeo ana mapenzi ya dhati
kwako, lazima atakupa kipaumbele na kufanya maamuzi sahihi kwa heshima na
sababu ya kuilinda ndoa yenu ambayo ni muhimu sana.
JIUNGE NASI
FB@EDONETZ TWITER@EDONETZ INST@EDONETZ_BLOG YOUTUBE@EDONE TV