China ni nchi ambayo inazidisha matumizi yake ya vioo kuunda vivutio vya kitalii kwa
kujenga choo cha vioo ambacho mtu anaweza akaona nje na hata ndani.
Ziwa Shiyan, katika mkoa wa
Hunan kusini mwa nchi hiyo.
Vioo hivyo vinawezesha wanaovitumia vyoo hivyo kutazama mandhari
ya kuvutia ya msitu au wengine wanaotumia vyoo jirani.
Aidha, walio nje wanaweza kuona walio ndani ya vyoo.
Kuta za vyoo hivyo, hata zile zinazotenganisha vyoo vya wanawake
na wanaume, ni za vioo kabisa ingawa vioo hivyo vimetiwa ukungu kiasi na Vyombo
vya habari nchini humo vinasema ni watu wachache sana waliotumia vyoo hivyo
siku ya kuzinduliwa kwake.
Licha ya umaarufu wa mijengo ya kutumia vioo katika ujenzi, hasa
kwenye madaraja na barabara, baadhi ya miradi imefungwa.
Habari za kuzinduliwa kwa vyoo hivyo zimevuma sana.hasa
mitandaoni ambapo wtu mbalimbali wametoa maoni tofauti tofauti juu ya hili.
Ejike Nnadi, alichangia katika ujumbe wa Facebook wa runinga ya
taifa CCTV amesema: "Hapana".
Ingawa kunao wengine wanaosema wanaweza kujaribu
kuvitumia.
Tina Chen anasema mradi huo wa vyoo ni ishara kwamba kuna mtu
alikuwa na pesa za "kupoteza".
Mi nirudi kwako mtu mkubwa msomaji wangu unaweza kuvitumia vyoo
hivyo vikija hapa bongo?