Kulijua jambo fulani lenye tija kwa undani ni vyema zaidi kwani itakusaidia kutambua kama unapaswa kuendelea nalo au lah, halikadhalika kwenye masuala ya kisheria watu wengi wamekuwa hawajui wafanye nini wawapo mahakamani kupitia Mtaalamu wa masuala ya kisheria Bashir Yakoub wanakuletea mambo kadhaa ya kuzingatia uwapo mahakamani, yapo 19 ila leo yapokee haya kama mengine katia toleo lijalo usisahau kuniandikia chochote hapo chini..

( 1 ) Kama  unahojiwa na  wakili mahakamani  usijibu  bila kutafakari alichokuuliza.

( 2 ) Wakili  asikuogopeshe kwa ukali  anapokuuliza  kwani  ukali hulenga kuleta paniki na kukusahaulisha  ulichopanga kusema.

( 3 ) Usilazimishe  kujibu kitu ambacho hukijui ni bora kusema  sijui kuliko kulazimisha kujibu.

( 4 ) Penda sana kujiamini  kwa kuwa kujiamini  hupunguza  uwezo wa  yule anayekuuliza, hata awe Jaji/Hakimu.

( 5 ) Jitahidi  kupata ushauri  wa wanaojua  sheria  kwa  kila hatua unayopiga  katika  kesi.

( 6 ) Kama wewe  ni  shahidi hakikisha unajadiliana  vya kutosha  na yule unayemtolea ushahidi  kabla  hamjaingia mahakamani.

( 7 ) Usipaniki kiasi cha kutoa neno  lolote la kashfa, kejeli, au  tusi mahakamani unaweza kuongeza kosa  la  kuidharau mahakama.

( 8 ) Katika kesi ya jinai usikubali kosa haraka kabla hujajua kitaalam kosa  hilo linaundwa na nini (vipengele vya kosa).

( 9 ) Kama  hukuelewa  vizuri  kosa  ulilosomewa  ni bora kukaa kimya, kwa kuwa ukikaa  kimya unaandikiwa umekataa kosa.

( 10 ) Kanuni  ya  sheria ni kuwa, ni kazi ya aliyekushitaki kuthibitisha kwa ushahidi kuwa umetenda kosa  na si kazi yako kuthibitisha kuwa  haujatenda  kosa



 
Top