Mama mjamzito huwa anaskia raha pale mtoto anapoanza kumpiga piga tumboni kwa mara ya kwanza. kucheza kwa mtoto kunafanya kuwa na mawasiliano mazuri kati ya mama na mtoto .Kwa wenye mimba ya kwanza mtoto ataanza cheza wiki ya 24 miezi (5-6), ila kwa wale walio zaa tayari mtoto mmoja au zaidi wanaskia mtoto akicheza akiwa wiki ya 18-22 mapema kidogo.
Kuna umuhimu wa mama kufatilia kujua
kucheza kwa mtoto,kwa kawaida watoto wanatakiwa wacheza mara
6 -10 ndani ya lisaa limoja (1hr) ile miezi 3 ya mwisho,na ile miezi
6 ya mwanzo kucheza kwake sio sana. Cha muhimu unatakiwa ujue pale anapocheza
na asipocheza.Kipindi cha usiku ndio muda wa watoto kupigapiga kuliko mchana
,na baada ya mama kula chakula pia huwa wapiga piga sana tumbo.
Sababu zinazompelekea mtoto kuto kucheza
: Mtoto kukosa nguvu za kutosha
kutokana na lishe mbaya ya mama yake,
:Mtoto hapati hewa ya kutosha kutoka
kwenye placenta
:Mtoto kuwa mdogo sana na uzito
mdogo nayo unamfanya ashindwe kucheza au akacheza kwa mbali sana na kukufanya
wewe usimskie kama anacheza.
:Mama anapokuwa na maradhi au
matatizo ya kiafya, hudhoofisha afya ya mtoto na kukosa nguvu
:Mama anapokuwa amechoka sana kwa
safari au kazi ngumu ,mtoto nae anakuwa anachoka na kuhitaji kupumzika na huwa
kimya sana
:Mama anapotembea sana au kusimama
kwa muda mrefu,kuna mfanya mtoto analale na kumfanya asicheze .
NJIA ZA KUMFANYA MTOTO ACHEZE TUMBONI
Mama anapohisi mtoto yupo kimya
anaweza kufanya yafuatayo..
:Kunywa maji baridi sana
:Kunywa juice
:kaa sehemu yenye makelele kama
ya radio,tv au washa vacuum cleaner
:Kula chakula au snacks -ataanza
kucheza
:Lala ulalie ubavu wa kushoto
:Kaa chini na unyooshe miguu juu ya
kitu
Iwapo ukatumia njia zote hizo na
bado yupo kimya ni vizuri ukawahi hospital ,hiyo ni ishara mbaya.
KUMBUKA . mtoto anapojinyoosha mwili, kukunja mguu
au mkono kunaweza msababishia mama kupata maumivu ,unatakiwa kupaka mafuta
ya maji tumboni na kulifanyia massage atajigeuza na maumivu yataisha.
ungana nasi ili usipitwe chochote
fb@edonetz,twiter@edonetz,inst@edonetz_blog na youtube@edone tv