karibu sana tuangalie ndoa leo tuanze na hivi hapa zingatia sana itakusaidia sana kwani watua walio wengi wanalalamika kila kukicha na wengine ndoa zinvunjika sana zingatia usipitwe hivihivi..


      1 Mjue make wako 
     Tambua mkeo ni wa aina  gani anapenda nini hapendi nini tambua tabia yake kama  anavumilia nyakati zote za shida na raha , Ukishamuoa ukaamua kuwa nae usipende kumuaidi vitu arafu usitimize hizo ahadi zitakughalimu kwani atitaji mpaka utimize kwahyo, usipotimiza unaweza kusababisha ugomvi mkubwa ndani ya familia .
      
      2 Uwezo wako 
Mwoneshe mwanamke mwisho wa uwezo wako ili atambue mapema asije akataka kitu kikubwa zaidi ya uwezo wako, na ukaanza kumlaum wakati hukumuonesha mapema au ulimwonyesha vitu ambavyo huna uwezo navyo .ukimzoesha kila siku kumpeleka matembezini au kumnunulia nguo nzuri kabla hujamuoa ukimuoa atakudai mpaka ugomvi kila siku ,pia mueleze kama una hela au huna atakuelewa na mtaishi vizuri  .
     3 HESHIMA 
   Mwanaume inabidi umueshimu mkeo kwa sababu hakuna mtu asiyependa kueshimiwa mheshimu sana naye atakueshimu  mwanaume tunza mkeo kwa heshima  mpe  atakachokiitaji kwa heshima  sio kisa  umemuoa unamtukana na kumyima raha hapo utasababisha ndoa ivunjike ,heshimu familia yako na ndo yako itadumu
  
    4 Usirudi nyumbani mikono mitupu,
    Nenda nyumbani na kijizawadi chochote kwasababu wanawake hupenda hata kikiwa  kidogo kulingana na uwezo wako kwani zawadi ni chochote beba hata pipi kwa akili ya mkeo na huo ndo upendo wa dhati.,urudipo nyumbani na chochote utapokelewa vizuri au mpelekee chochote unachojua mkeo anakipenda sana huko ndo kupalilia upendo .
    5 Tunza familia yako ipasavyo 
     
       Kwa habari ya imani tunajua kwamba mwanamke ametoka kwenye ubavu wa mwanaume kwa hiyo mwanaume ni kichwa ndani ya familia . Mwanaume ukitambua hilo ,utatunza familia yako vizuri kwa umakini kwa sababu mwanamke ni msaidizi lakini mnampa mizigo mizito ndani ya familia . Sio kupenda kula tu huku hujatoa hata mia tambua kua huo ni wajibu wako na kila kitu ndani ya familia kinakuhusu na inabidi ukisimamie au ukabiliane nacho .
     unaweza kuzingatia hayo yatakusaidia sana katika maisha yako na ndoa yako kiujumla na mausiano karibu sana @mtumkubwa usisahau kulike page yetu facebook, inster na twiter @edonetz
 
Top