Msami et Barakah da Prince hana nguvu ya kuwa mume wa
Naj
Msanii wa muziki na mwalimu wa dance, Msami
Giovani anayefanya vizuri na wimbo wake ‘Step by Step’ amesema Barakah The
Prince bado hana nguvu ya kuwa mume wala kuwa mchumba wa Najma.
Ametoa kauli hiyo baada ya Barakah kumtukana
Msami baada ya kukoment katika akaunti ya Instagram ya Naj.
Akiongea na E-News ya EATV, Msami alisema,
“Kwanza Barakah ajue Naj sio mke wake, wala mchumba wake ni boyfriend na
girlfriend tu. Kwahiyo Barakah hana nguvu ya mume wala mchumba kwa Naj. Kwahiyo
hata mtu mwingine anaweza kuleta fujo na kutupa kete yake. Halafu mie ni
expensive sana kwa Naj watu ambao naweza kurusha kete yangu kwa watu ambao ni
expensive ambao wapo kwenye level yangu kama mimi. Naj yupo kwenye level ya
Barakah na mimi nipo kwenye level nyingine kabisa za juu. We angalia watu wangu
awe Uwoya au Kajala, kwahiyo mimi ni expensive sana.”
AliKiba na Mr Blue waungana kumrudisha Abby Skills
Msanii ambaye alifanya vizuri kipindi cha nyuma
na nyimbo ‘Maria’ na ‘Mimi na Wewe’ Abby Skills anajipanga kurudi upya katika
game la muziki na wimbo ‘Averina’ akiwa na Ali Kiba.
Muimbaji huyo amesemaa kuwa AliKiba na Mr Blue
ndiyo watu ambao wanamsimia kwa sasa ili kumrudisha upya kwenye chati.
“AliKiba na Mr Blue walikaa chini na kuamua
kunisaidia kunirudisha kwenye game,” alisema Abby. “Waliniambia tumeona una
kipaji kizuri, una melody ngoja tushirikiane ili kukupeleke sehemu fulani,”
Aliongeza, “Hata hii project yangu mpya na AliKiba
‘Averina’ wao ndio wanasimamia kila kitu, kwa hiyo kuna mambo mazuri yanakuja
hivi karibuni,”
Muimbaji huyo amesema kazi yake mpya
aliyomshirikisha AliKiba itatoka hivi karibuni kwa kuwa tayari ameshashoot na
video.
Ukimya wa muda
mrefu
Ray C’ Chalamila’ uko mbioni kuzimwa kwa
kishindo
Ukimya wa muda mrefu wa Rehema ‘Ray C’
Chalamila’ uko mbioni kuzimwa kwa kishindo. Ni kwasababu mwanamuziki huyo
mkongwe, ameingia studio za Wanene Entertaiment jijini Dar kurekodi kazi mpya.
Muimbaji
huyo ambaye kwa muda mrefu amekuwa akipambana na uraibu wa madawa ya kulevya,
amepata mshirika mjuzi wa kumuongoza katika mrejeo wa nguvu – Damian Soul.
all the best ray c
Mr Nice kwanini anakubalika Kenya?
Mwanamuziki, Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ amesema
ukongwe wake kwenye muziki ndiyo kitu ambao kinampatia mashavu zaidi nchini
Kenya.
Alhamisi hii, Mr Nice amesema Kenya ni sehemu
pekee ambazo anaweza kufanya show nyingi bila mashabiki kumchoka.
“Najivunia kuwa rafiki namba moja wa Wakenya,”
alisema Mr Nice. “Hiyo ni silaa yangu kubwa katika muziki wangu, kwa hiyo labda
ni kwa sababu tayari tumeshatengeneza chemistry nao toka naanza kufanya
muziki,”
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na albamu
yake ya Kioo, hivi karibuni alijaza umati wa mkubwa katika show yake
iliyofanyika katika club moja huko nchini Kenya.
Muimbaji huyo ijumaa hii atakuwa mjini Kisumu
na Jumamosi atakuwa katika jiji la Nairobi maeneo ya Embakassy katika muendelezo
wa show zake.
mashabiki wa Afrika Kusini wanahamu na Raymond kwenye
MTV MAMA 2016
Jumamosi hii ya Oktoba 22, mwaka huu
zinatarajiwa kufanyika tuzo za MTV MAMA 2016 kwenye ukumbi wa Ticket Pro Dome,
Johannesburg, Afrika Kusini lakini imedaiwa kuwa Raymond ameonekana kuvutia
zaidi kwenye tuzo hizo.
Mtangazaji anayefanya vizuri kwa sasa kupitia
Times FM na kipindi chake cha The Playlist, Omari Tambwe aka Lil Ommy ambaye
ameweka kambi nchini humo kwa ajili ya kushuhudia tuzo hizo amesema kuwa
mashabiki wamekuwa wakiwasubiri wasanii wengi lakini shauku yao kubwa ipo kwa
Raymond wa WCB.
“Wanasubiriwa wasanii wengi lakini, shauku
zaidi ipo kwa Raymond watu wengi hapa wameanza kumfuatilia, wengine wakiwa na
hamu ya kumshuhudia kuzingatia ni msanii mpya halafu kipengele chenyewe kina
uzito yaani msanii aliyeingia na kufanya vizuri,” Lil Ommy ameiambia Times FM.
Raymond anawani kipengele cha msanii bora
anayechipukia, wao wanakiita Best Breakthrough Act akiwa na wasanii wengine
kama Simi (Nigeria), Nathi (Afrika Kusini), Nasty C (Afrika Kusini), Franko
(Cameroon), Falz (Nigeria) na Emtee (Afrika Kusini).
Feza Kessy anahisi Nando anadata
Staa aliyewahi kuiwakilisha Tanzania katika
shindano la Big Brother Africa, Feza Kessy, amesema kuwa anaamini Nando
aliyewahi kushiriki naye kwenye shindano hilo, amepatwa na tatizo au anaugua
kwakuwa tabia anazozionyesha zinampa mashaka.
Akiongea kwenye kipindi cha Kubamba kupitia
Times FM, Feza amesema anaona akili ya Nando kama imevurugika kwa sasa. Anasema
amekuwa tofauti na Nando, yule kijana mwenye nidhamu na mpole aliyekuwa
akimfahamu.
“Naamini Nando ana tatizo asaidiwe,” alisema
Feza. “Sijui kwanini lakini naamini Nando ana something hayupo sawa, sio yule
Nando ninayemfahamu, naomba atafutwe asaidiwe,” alisisitiza.
Feza ambaye kwa sasa ni mtangazaji wa Choice
FM, amedai kuwa aliwahi kukutana na Nando na akampa noti ya shilingi elfu 10.
Anasema badala yake yake staa huyo aliitupa chini kwa madai kuwa haiwezi
kumsaidia kitu.
..................................................................
Vanessa Mdee amezidi kutanua jina lake nchini
Nigeria. Wimbo alioshirikishwa na rapper wa Nigeria, Ice Prince ‘No Mind Dem’
umefanikiwa kuwa moja kati ya nyimbo zitakazopatikana kwenye albamu mpya ya
rapper huyo ‘ ‘Jos To The World’.
Ice Prince anatarajia kuachia albamu yake hiyo
ya tatu Oktoba 28, mwaka huu baada ya ile ya ‘Everybody Loves Ice Prince’ na
‘Fire of Zamani’ ambayo itakuwa na nyimbo 18.
Ndani ya albamu hiyo amewashirikisha wasanii
wengine kama Phyno, Tiwa Savage, Run Town, Yemi Alade, Dj Buckz na wengine.
Mwanamuziki nguli wa Kenya Achieng Abura afariki dunia
Mwanamuziki mkongwe wa nchini Kenya na
aliyewahi kuwa Principal kwenye mashindano ya Tusker Project Fame, Achieng
Abura amefariki dunia.
Kwa mujibu wa The Standard, amefariki Alhamis
hii kwenye hospitali ya taifa ya Kenyatta jijini Nairobi. Bi. Abura alikuwa
amelazwa katika wodi binafsi akitibiwa ugonjwa ambao haujajulikana.
Bi. Abura Alifariki dunia mida ya saa 12 jioni.
Mapema mwezi huu, muimbaji huyo aliandika kuwa afya yake si nzuri na madaktari
walimshauri aongeze uzito kisha kuupunguza kupitia mazoezi.
Chanzo cha karibu na familia yake kilidai kuwa
alihamishwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi baada ya hali yake kuwa mbaya.
Wasanii mbalimbali wa Kenya wametuma salamu zao
za rambirambi kupitia mitandao ya kijamii. Hawa ni baadhi yao.
Avril
My day ends on a sad note..don’t know what to
say…RIP Achieng Abura :'( ..
Nameless
So sad to hear of your passing dear
sister….Rest in peace Achieng Abura.
Akothee
You’ve done your part….it’s a journey…I mourn
you ! RIP #RIPAchiengAbura
Sauti Sol
Our heartfelt condolences to the family and
friends of the late Achieng Abura. She was a natural talent, mentor to us all.
This is a big blow to the music industry! #Rip #RipAchiengAbura #Shujaa
The King Kaka
Rest In Peace.
Achieng Abura.
Safiri Salama, tutaonana Baadaye.
Achieng Abura.
Safiri Salama, tutaonana Baadaye.
Amani
R.I.P. Achieng Abura
…a lovely woman who was
passionate about music #legend