Na Involatha  Beningnus - edonetz
kila mmoja hapa ulimwenguni anaitaji kufanikiwa ila wengine ujikuta wakitumia dhana potofu ili kupata mafanikio ila kwakutumia mungu lazima ufanikiwe ukifuatilia vizuri yafuatayo...

1  Tii sheria za Mungu 
Sheria za Mungu ni maagizo yake  atuagizo tutende maagizo hayo ni neno la lake .Jifunze sheria kupitia  wafuasi wa Mungu  kwenye Biblia kwa mfano Mussa, Yusuph , n.k walivyotii sauti  na sheria pia. Mtu wa Mungu lazima malengo yako yatimie endapo utatii neno la Mungu , lakini utambuapo umekosea kwa aina yoyote rudi nyumba ukaombe toba naye atakusikia . Tunza malengo yako yasichukuliwe na mwovu shetani kwa kutii sheria zake ,kusoma bibilia maana ukiwa na neno shetani hawezi kukushinda .


        2 Tunza siri 
Unapopewa maono usimwambie kila mtu, maana wengine ni vibaraka wa shetani . Vyema unapopata maono uwe msiri kuna maono mengi  ni yako na Mungu na Biblia inatufundisha kua sio maono yote unaweza kuwashirikisha watu. Mfano tunamuona Yusuf alipowaeleza ndugu zake kwa habari ya ndoto yake walimwonea wivu wakataka kumuua . Kabla ya kumwambia Mtu  yeyote Muulize Mungu, zungumza na Mungu ,akikuzuia usimwambie Mtu kaa kimya . Wapo  watu wanaweza kupigana na maono yako kwa sina mbalimbalina kusababisha maono yako yasifanikiwe.
             
         3 Uaminifu kwa kazi za Mungu 
Uamnifu kwa Mungu ni muhim sana maana ukuweka karibu na Mungu pia kukuweka huru kwa mfano maombi kwa waitaji ,kuombea nchi yako na watu wote kwa ujumla , kuwaona yatima wajane na wagonjwa ukifanya hivi Mara kwa Mara Mungu atainuliwa kupitia wewe. Pia kila mtu  ana karama yako jaribu  kutumia vizuri karama yako kwa mfano kuimba , kucheza, kuhubiri au kutangaza injiri kama ukifanya hivo Mungu atajidhihirisha kwako pia atakuinua wew na vizazi vyako vyote
       . 4 Matoleo kwa Mungu 
Sheria moja wapi kwa Mungu ni matoleo maana kuna nataka tele kwa wale wamtoleao na laana  kwa wale wasiomtolea .Biblia inatueleza kwamba umtoleapo zaka Mungu atamzuia na kumkemea yule alaye maana yake ni kwamba  labda mkuu wako wa kazi anataka akupandishe  cheo au wewe ni mwanfunzi inabidi ufaulu na pia kwenye biashara kufanikiwa ,kwakua humtolei Mungu mambo mengi yatainuka kwa mfano magojwa ,kukata tamaa ,vishaishi vibaya kesi mbalimbali pengine  hujafanya wew hapo shetani anakua amekula maono yako , mtolee Mungu ili ubarikiwe na usonge mbela bila kikwazo na usonge mbele ili ubarikiwe wewe na familia yako na chochote utakachokigusa kitabarikiwa
         5 Maombi ya kumaanisha 
Wapendwa tusiombe kwa mazoea maana hata Biblia unatuzuia kwa habari ya mzaa ishi ndani ya maombi kwa kumwelezaMungu mambo mbalimbali mabaya kwa mazuri pia shukuru kwa yote utakayopata.Mungu uamua kujibu au asijibu kulingana na haja yako au maombi yako eidha umekosea kuomba au unafanya mzaa , unaomba kwa mazoea ,omba toba kwanza ndipo  umueleze Mungu maombi yako .
        6 Upendo kwa wote 
Biblia inatueleza kua Amri kuu ni upendo je umemsaidiaje ndugu yako alivokueleza shida yako? Mpokee kwa upendo kwa sababu Mungu uwatumia watu mbalimbali kuleta baraka  ,mashuleni,kazini kwenye biashara yako , jifunze kuishi na watu  vizuri wanaweza kukusaidia pindi unapoitaji msaada kwa mfano kufikia ndoto zako au malengo yako.,pia jifunze kutoa  kwa sababu biblia itwambia ni kheli kutoa kuliko kupokea ,kumbuka ukimsaidi mtu  Leo wewe utapewa kesho zaidi ya pale. 
      
        Mungu ni mwaminifu akubariki ili utende yampendezayo

 mtumkubwausikose kulike kurasa zetu za facebook,twiter na inster @edonetz
 
Top